![]() |
KOCHA WA MANCHESTER UTD JOSE MOURINHO |
MOURINHO
Mourinho ameshitakiwa kutokana na matamshi yake juu ya Refa Anthony Taylor ambae Wiki iliyopita alichezesha pambano la Liverpool na Man United huko Anfield na kwisha 0-0.
Uamuzi huo wa FA umekuja baada ya Chama hicho kuona amevunja Sheria kwa kuongea kuhusu Marefa kabla ya Mechi wanayopangiwa.
Mara baada ya Refa Taylor, mwenye Miaka 37 na anaetoka Kitongoji cha Wythenshawe kilichopo Maili 6 tu toka Old Trafford Nyumbani kwa Man United huko Jijini Manchester, kuteuliwa kuliibuka malalamiko, na hasa Mashabiki wa Liverpool, ambao walilivalia njuga kwenye Mitandao ya Kijamii.
Hata Keith Hackett, Refa wa zamani na Mkuu wa zamani wa Kampuni ya Marefa PGMOL, alisema kutaibuka malamiko makubwa ikiwa Refa huyo atafanya kosa lolote kwa upande wowote ule.
Akiongea na Wanahabari kabla ya Mechi hiyo na Liverpool, Mourinho aliulizwa kuhusu uteuzi wa Refa huyo na yeye kujibu: “Nadhani Bwana Taylor ni Refa mzuri sana lakini anapewa presha kubwa na itakuwa ngumu kwake kuwa na kiwango kizuri cha kuchezesha.”
Aliongeza: “Sitaki kuzungumza mengi kuhusu hili. Ninayo maoni yangu lakini nishapata fundisho kwa kuadhibiwa mara nyingi kuhusu kauli zangu kwa Marefa!”
FA sasa imemshitaki Mourinho kwa kuvunja Sheria iliyotungwa Mwaka 2009 inayokataza Mameneja kuongea lolote kuhusu Marefa kabla ya Mechi na amepewa hadi Oktoba 31 kujibu Shitaka la Utovu wa Nidhamu na kuiingiza Gemu kwenye Jina baya.
Meneja wa kwanza kabisa kusulubiwa kwa Sheria hiyo alikuwa ni Meneja wa zamani wa Man United, Sir Alex Ferguson, ambae alishitakiwa Mei 2011 kwa kutoa kauli kuhusu Refa Howard Webb ambayo haikuwa mbaya bali ilikuwa ya kumsifia pale aliposema alikuwa ni Refa Bora huko England.
Katika Mechi hiyo ya Man United na Liverpool ya Wiki iliyopita, Refa Anthony Taylor alitoa Kadi za Njano 4 na zote zilikwenda kwa Wachezaji wa Man United.
MOYES
NAE David Moyes wa Sunderland ameshitakiwa na FA kwa Kosa la kutumia Lugha ya Matusi kwa Waamuzi wa Mechi ya Raundi ya 4 ya EFL CUP huko Saint Mary ambako Sunderland walifungwa 1-0.
Tukio linalomhusu Moyes lilitokea Dakika ya 90 baada ya Refa Chris Kavanagh kuikataa Penati ya Sunderland baada ya Mchezaji wao Victor Anichebe kuchezewa Faulo.
Moyes, akiwa pembeni mwa Uwanja, alipandwa na Jazba na Refa huyo kumtoa nje ya Uwanja.
Moyes, ambae aliteuliwa kuwa Meneja wa Sunderland Mwezi Julai na ambae ameambua Pointi 2 tu katika Mechi 9 za Ligi, amepewa hadi Oktoba 31 kujibu Shitaka lake.
EPL - LIGI KUU ENGLAND
**Saa za Bongo
Jumamosi Oktoba 29
1430 Sunderland v Arsenal
1700 Man United v Burnley
1700 Middlesbrough v Bournemouth
1700 Tottenham v Leicester
1700 Watford v Hull
1700 West Brom v Man City
1930 Crystal Palace v Liverpool
Jumapili Oktoba 30
1630 Everton v West Ham
1900 Southampton v Chelsea
Jumatatu Oktoba 31
2300 Stoke v Swansea
No comments:
Post a Comment