EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, December 5, 2013

MAN U HALI MBAYA WAKATI, RVP HAIJULIKANI LINI KURUDI UWANJANI!!

Moyes unsure over Van Persie return 

INGAWA Meneja wa Manchester United David Moyes amedai maumivu ya Robin van Persie si kitu cha kutisha na kikubwa lakini ameshindwa kutaja ni lini Staa huyo atarudi dimbani kuiokoa Man United ambayo Jumamosi itacheza bila ya nguzo yao muhimu Wayne Rooney.


Van Persie ameshazikosa Mechi 4 za Man United akijiuguza maumivu ya Nyonga na mara ya mwisho kucheza ni pale alipoitungua Klabu yake ya zamani Arsenal ambayo ilifungwa Bao 1-0 kwa Bao lake.

Tangu Van Persie akose Mechi hizo 4, Man United imeambua Pointi 2 tu katika Mechi 3 za Ligi ingawa waliichabanga Bayer Leverkusen Bao 5-0 kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI huko Ujerumani.

No comments:

Post a Comment