NA: KASSIM NGUMBI
 |
| Naibu KTB Mkuu..CCm..Mwigulu Nchemba |
Akizungumzia Kuelekea Katika Bunge La Katiba, Wakati Wa Ziara Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara Hapo Jana, Naibu Katibu Mkuu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Mwigulu Nchemba Amesema Kuwa Utekelezaji Wa Suala Hilo Ni Katika Kusimamia Ilani Ya Chama Hicho, Hatua Kwa Hatua, Ili Iwe Njia Sahihi Ya Kufikia Maelewano Na Hatimaye Maendeleo Endelevu.Katika Ziara Hiyo Ambayo Aliweza Kufungua Mashina Mbalimbali Ya Wakereketwa Akiwa Wilayani Tandahimba Na Kugawa Kadi Kwa Wanachama Wapya, Amewataka Wananachi Kujiunga Na Chama Hicho Ili Kwa Pamoja Kuweza Kutengeneza Ajenda Za Maendeleo, Akieleza Kuwa Msingi Wa Mambo Yote Ndani Ya Chama Hicho Ni Kazi.Katika Hatua Nyingine Naibu Katibu Mkuu Huyo Ambaye Pia Ni Mbunge Wa Jimbo La Iramba Mashariki Mkoani Singida, Amewatoa Hofu Wakulima Wa Zao La Korosho Kuwa Serikali Iko Bega Kwa Bega Katika Kuhakikisha Inasimamia Vyema Mfumo Wa Ununuzi Wa Zao Hilo Na Wakulima Kupata Malipo Ya Pili Ya Mauzo Ya Zao Hilo.Mwigulu Nchemba Katika Ziara Hiyo Aliweza Kugawa Kadi 316 Kwa Wananchama Wapya, Na Pia Kufungua Matawi Matatu Ya Wakereketwa, Na Kushiriki Katika Kampeni Za Udiwani Katika Kata Ya Mkwiti Wilayani Tandahimba.
SIKILIZA HOTUBA YAKE HAPA...............
No comments:
Post a Comment