EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, December 5, 2013

PELE KUKATAA KUWEPO KATIKA DROO YA UPANGAJI RATIBA.HATUA YA MAKUNDI KOMBE LA DUNIA


 GWIJI wa soka duniani, Pele hatashiriki droo ya upangaji ratiba ya Kombe la Dunia itakayofanyika Leo, baada ya kukataa fursa hiyo akihofia kuiweka Brazil katika kundi gumu.  Pele amesema atakuwepo kushuhudia zoezi hilo lakini amethibitisha hatashiriki. Nguli aliendelea kudai kuwa rais wa Brazil Dilma Rousseff alimpendekeza aiwakilishe nchi hiyo litakapokuja zoezi la kuchagua timu na kuweka katika makundi kazi ambayo ameifanya mara kadhaa.  Pele amesema ameamua kukataa kwasababu asingejisikia vyema kuchagua timu ambazo zitaiweka Brazil mahali pagumu. Droo ya kupanga ratiba ya michuano hiyo itakayoanza kutimua vumbi Juni 12 mwakani itashirikisha nchi 32 kutoka sehemu mbalimbali duniani.

No comments:

Post a Comment