Kaimu Katibu wa Zurkhaneh Tanzania Abdallah Nyoni |
NA MSHAMU NGOJWIKE
WACHEZAJI wa mchezo wa ngumi unaofahamika kama
Zurkhaneh wameondoka hii leo kwenda nchini Iran kwenye mashindano ya Dunia
ambayo yataanza kuchezwa Oktoba 30 hadi Novemba 3.
Mashindano hayo yatashirikisha nchi 25 wanachama wa mchezo huo,huku
Afrika zikiwakirishwa za Tanzania,Kenya,Uganda, Msumbiji,Benin,Zambia na
Zimbabwe.
Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Katibu wa Zurkhaneh Tanzania Abdallah Nyoni amesema vijana hao
wametoka asubuhi ya leo kuelekea nchini Iran ambako kutafanyika Mashindano hayo
kwenye Mji wa Lorestan huku wakiwa na murali ya kurudi na ushindi kutegemeana
na mazoezi waliyofanya.
Alisema mwaka huu kwenye fainali hizo zitawakilishwa
na Mwarabu Mirundi pamoja na Patrick Ntakisigaye kutoka kwenye klabu ya
Mianzini zurkhaneh iliyopo Mbagala Dar es Salaam.
Mashindano hayo ya Zurkhaneh kwa upande wa Koshti Pahlavani yameandaliwa
na nchi ya Iran ambayo yamedhaminiwa na International Zurkhaneh sports
Federation(IZSF).
No comments:
Post a Comment