|
JAM WEEEZY msanii wa bongo freva anayekuja |
MSANII Juma Omary maarufu kama JAM WEEZY mwenye umri wa miaka 21 mkazi
wa mkoani mtwara ameiambia Swacotz forum kuwa yuko mbioni kuachia ngoma
yake mpya itakayojulikana kwa jina la harakati,nyimbo ambayo amesema
anatarajia kuifanya kwenye studio za Suri hapahapa mjini mtwara katika
maelezo yake Jam Weezy ambaye ametamba mkoani mtwara na nyimbo ya
CHAPCHAP aliyoimba na wasanii wenzake wa kundi la NON DISPEAR la mkoani
humu pamoja na kushirikishwa kayika nyimbo ya msanii wa musiki aina ya
RAGGER DOT KADIO nyimbo iitwayo SPEED amesema kwa sasa amejipanga na
ameamua kufanya muziki hivyo wasanii wengine waliotangulia wakae mkao wa
vita dhidi yake kwani tayari amekwishaandika mashairi mengi sana mazuri
na anaamini akiyaingiza sokoni yatafanya vizuri. licha ya msanii huyo
kuwa na nyimbo chache lakini amekuwa ni msanii anayekubalika sana mkoani
mtwara huku nyimbo zanazosikika sauti yake zikipendwa na vituo vyote
vya radio vilivyopo mkoani hapa mwisho Jam weezy amemaliza kwakuwataka
watanzania wote wampokee na kumpa sapoti ya kutosha katika kazi zae.
No comments:
Post a Comment