Imeelezwa
kuwa ni vizuri wananchi wa manispaa ya mtwara mikindani wakajitoa zaidi kwenye kilimo,
ili kuondoa tatizo la baa la njaa, ambalo limeanza kujitokeza kwa majirani zetu
wa mkoa wa lindi.
Hayo
yamesemwa na wananchi tofauti tofauti wakati wakizungumza na mwandishi wa habari
wa pride fm radio mapema hii leo asubuhi, ambao wamesema kuwa tatizo ambalo linaanza
kuonekana mkoa wa lindi linaweza kufika mkoani mtwara hivyo ni vizuri kujipanga
mapema kwa ajili ya kukabiliana na tatizo hilo.
Baadhi
ya wananchi waliozungumza na pride fm radio akiwemo godfrey namohochi wa manispaa
ya mtwara mikindani amesema kuwa kila mwaka nchi huwa inaingia kwenye janga la
njaa, tatizo ambalo husababishwa na wananchi kutojikita katika kilimo.
Mkazi
mwingine mkata juma amesema kuwa kutokana na kutozalisha tunaendelea kuilaumu serikali
kuwa haitoi misaada hivyo akawaomba wananchi kujikita
katika kuzalisha mazo kutokana na msimu wa mvua kuanza hali ambayo itatutoa kwenye
majanga ya kutokuwa na chakula cha kutosha.
Naye
juma hamisi amewataka wananchi wenzake kuwa waelewa na kufuata ushauri na elimu
inayotolewa na wataalamu wa kilimo ili kujikwamua kiuchumi na hata kuondoa janga
la njaa ambalo huwa linajitokeza mara kwa mara na kupunguza mzigo kwa serikali.
No comments:
Post a Comment