EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Saturday, August 16, 2014

Ndanda yakabidhiwa vifaa

NA MSHAMU NGOJWIKE
TIMU ya Ndanda , jana imekabidhiwa msaada wa  vifaa vya michezo kutoka kwa Kampuni ya Gesi ya BG Tanzania ya   Mtwara .

Vifaa hivyo vimekabidhiwa kwa ajili ya kutumiwa katika maandalizi ya Ligi Kuu soka Tanzania bara inayotarajia kuanza Septemba 20.

Vifaa vilivyokabidhiwa  na Meneja Kampuni hiyo  Adam Prince ni Viatu, Mipira 20 aina ya Brazuka, Jezi pea 30, jaketi  30,traki suti za mazoezi pea 30.

Pia, alisema watakabidhi basi jipya aina ya Toyota lenye uwezo wa kubeba wachezaji 30 ifikapo Novemba mwaka huu, mara baada ya kufika  nchini.

Akizungumza katika Hafla ya kukabidhi vifaa hivyo, Meneja huyo alisema wanajisikia faraja kupokelewa vizuri  Mtwara,  wanataka kuifanya Ndanda kuwa timu  tishio kwenye  msimu wa ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Tumefanya hivi kujiweka karibu na jamii, nakuifanya Klabu ya Ndanda kuwa miongoni mwa timu tishio kwenye msimu mwa huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara,”alisema.

 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia amewataka wachezaji pamoja na wadau wengine kujitokeza kuisaidia timu hiyo ili ifanye vizuri kwenye msimu wa Ligi Kuu mwaka huu.

“Ninawashukuru BG Tanzania kwa Msaada wao huu,hii ni kuonyesha jinsi gani wanavyothamini watu wao wa Mtwara,ninawataka na wadau wengine kuisaidia timu yetu,”alisema.

Ndanda FC ipo jijini hapa, imeweka kambi ya siku 40,kwenye  Chuo Cha Kikuu Cha Ardhi ikijiandaa na Ligi kuu Msimu ujao.

Wanariadha wa Tz kurekebisha rekodi michuano ya Kitaifa
i

No comments:

Post a Comment