EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Saturday, August 16, 2014

Wanariadha wa Tz kurekebisha rekodi michuano ya Kitaifa

NA    NYEMO MALECEL
WANARIADHA wa Tanzania wamepanga kuyatumia mashindano ya majeshi ya Afrika Mashariki yanayotarajia kuanza keshokutwa  Zanzibar kurekebisha rekodi za muda wao kitaifa.
Akizungumza na SWACOTZ FORUM jana Katibu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui alisema mashindano hayo hayatambuliwi na Shirikisho la Riadha la Kimataifa (IAAF) lakini ni fursa nyingine kwa wanariadha wa Tanzania walioajiliwa na Taasisi za vyombo vya Ulinzi na Usalama kujipima nguvu kwa Wakenya na Waganda.
Nyambui alisema RT sio msemaji wa mashindano hayo lakini inachokijua ni kwamba ni mashindano muhimu  kwa taasisi za jeshi hivyo lazima yatawashirikisha wanariadha wa wenye uwezo mkubwa ili kuhakikisha kila chombo cha ulinzi na usalama kinapata ushindi.
“Japokuwa mashindano hayo hayaingiliani kabisa na RT lakini ni muhimu kwetu maana tuna uhakika kila jeshi limewaandaa vizuri wanariadha wake ili kuhakikisha wanafanya vizuri jambo ambalo litawasaidia kurekebisha muda wao wa ndani,” alisema.
Alisema hakuna wanariadha anayetaka kufungwa ila cha msingi wanatakiwa kurekebisha muda wao kwa kujipima nguvu na wakimbiaji mashuhuri kutoka Kenya na Uganda ambao wamekuwa wakifanya vizuri katika michuano ya kimataifa.

No comments:

Post a Comment