EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, August 21, 2014

UNYAMA WA KUTISHA IRINGA MWANAFUNZI AUA MTOTO WAKE WA SIKU MOJA AMHIFADHI KATIKA MFUKO WA RAMBO

mwanafunzi aliyetupa mtoto
Na Mathias Canal-Iringa
mtoto  akiwa  amehifadhiwa  ktik mfuko  wa  rambo

hapa  ndipo alipofichwa  mtoto  huyo
Hivi ndivyo  mwanafunzi huyo alivyomhifadhi mtoto  huyo
Mwenye chumba akiomba msamaha
Damu ya  mtoto  huyo aliyeuwawa
Polisi  wakimhoji binti mwenye  chumba
Hii ndio  nyumba ambayo  binti  huyo alikuwa akiishi mwenye nyumba akiwa chini ya ulinzi akitolewa nje ni huyo mwenye sweta
Watuhumiwa  wakitolewa katika  chumba  hicho
Polisi  wakiweka  ulinzi mkali.

Mwanafunzi huyo akipanda katika gari  la polisi
Mwanafunzi huyo akiwa na mwenyeji  wake  kushoto
Huyu ndie  binti  mwanafunzi aliyetuhumiwa kufanya mauwaji
Wananchi  wakimtazama  mwanafunzi huyo
Mwanafunzi Vema  Mtati wa chuo cha unesi Chimala wilayani Mbarali mkoani Mbeya akamatwa na polisi mkoani Iringa kwa tuhuma za mauwaji ya mtoto wa siku moja aliyejifungua salama.

Tukio hilo la kinyama limetokea leo saa 12 jioni  katika  eneo la Kijiweni kata ya Mvinjeni Manispaa ya Iringa kutokana na baadhi ya majirani kufichua siri hiyo nzito ya kuwepo kwa jaribio za binti huyo kufanya mauwaji hayo. 


Mmoja kati ya majirani aliueleza kuwa binti huyo mwanafunzi akiwa na mimba ya miezi tisa alifika katika nyumba hiyo kwa rafiki yake ambae ni mfanyakazi wa bar mmoja eneo la vibanda vya CCM mjini Iringa aliyefahamika kwa  jina la Joys siku kama tano kabla ya usiku wa jana kujifungua salama katika chumba hicho.


Shuhuda  huyo  alidai kuwa mapema  asubuhi ya  leo  walisikia  sauti ya  mtoto  mchanga akilia   huku sauti ya radio  ikipandishwa  kupoteza  sauti ya  mtoto  huyo  ili  wapangaji  wengine  wasijue suala  hilo.

Hivyo  kutokana na hali  hiyo ndipo waliamua  kufika  ofisi za mtandao huu kufichua siri hiyo kwa maombi ya kutotajwa popote  jina la  shuhuda  huyo.

" Mimi ni  raia mwema na mwanamke  mwenye  uchungu  nimekuja kwako huku  nikijua hutatoa siri  hii ...katika  nyumba ambao naishi  kuna  mwanafunzi amejifungua mtoto jana usiku na kwa  sasa amejifungia ndani na  mwenye chumba anaitwa Joys anafanya kazi  vibanda  vya CCM sasa  lengo  la kujificha nafikiri ni kutaka  kufanya jaribio la kuua mtoto  huyo  sasa naomba usaidie  kuokoa maisha ya mtoto  huyo unatusaidiaje na sisi kwenda  polisi tunaogopa ushahidi"

Kutokana na maelezo hayo  yasio na chembe  ya uongo mtandao  huu ulipiga  simu kwa OCD Iringa Bw Pyuza na  bila  kuchelewa kikosi kazi  akiwemo askari wa dawati la jinsia  kilifika  katika ofisi  za mtandao  huu wa matukiodaima na safari ya  kufuatilia  suala  hilo  ilipoanza kwa kumkamata mwenyeji wa mwanafunzi huyo ambae ni mmiliki wa  chumba kisha  kupokonywa  simu yake ili asifanye  mawasiliano nyumbani na baada ya hapo kwenda katika nyumba  husika .


Hata  hivyo ukweli wa jambo ulianza kujionyesha baada ya kufika katika  chumba  hicho na  kukuta mlango  umefungwa kwa ndani na baada ya  mwenye chumba kugonga ndani mwanafunzi huyo aliigiza kuwa alikuwa akifanya usafi  ila baada ya  kuhojiwa na polisi alidai kuwa kwa sasa ana mtoto mmoja ambae  yupo  kijijini Magulilwa  wilaya ya Iringa .

Uchunguzi wa  kipolisi ulianza na kikosi  hicho kwa maswali ya kiuchunguzi na ndipo alipokiri kuwa anamtoto mwingine ambae amejifungua usiku wa  leo na amemhifadhi  katika mfuko wa rambo ndani chini ya kitanda .

Alipotakiwa  kumtoa  alifanya  hivyo na polisi  na mmiliki wa mtandao  huu kushindwa  kujizuia kuangua  kilio kutokana na kile  walichokiona  kutoamini .
Mtoto  huyo alikutwa amekufa huku akiwa amefungwa na  nguo nyingi  pamoja na kumwagiwa vumbi ya mkaa na chumvi  ili asitoe harufu na kufungwa  vizuri katika mfuko wa rambo mweusi  kisha kuwekwa katika mfuko mkubwa wa  salfeti tayari kwa  kuvuta  subiri ya kwenda kumtupa mtoto  huyo porini .

No comments:

Post a Comment