EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Tuesday, July 15, 2014

CBF: SHIRIKISHO LA SOKA BRAZIL: SI KWELI KWAMBA SCHOLAR KAFUKUZWA BRAZIL

PrintPDF
BAADA Magazeti huko Brazil kutapakaza habari za kutimuliwa kwa Kocha wa Brazil Luiz Felipe Scolari hapo Jana, hatimae CBF, Shirikisho la Soka la Brazil, limetoa tamko kwamba Kocha huyo ameamua kuiacha nafasi SCOLARI-AFUNIKA-USOyake.
Hata hivyo, Mkataba wa Scolari ulikuwa unamalizika mara baada ya Fainali za Kombe la Dunia kuisha.
Tangu wachapwe 7-1 na Germany kwenye Nusu Fainali ya Kombe la Dunia Wiki moja iliyopita, Magazeti huko Brazil yalitaka Scolari aondolewe lakini Kocha huyo alisema hatima yake iko mikononi mwa CBF na kuendelea kuiongoza Brazil kwenye Mechi iliyofuatia ya Mshindi wa Tatu wa Kombe la Dunia ambayo walichapwa 3-0 na Netherlands.
Scolari ndie aliekuwa Kocha wa Brazil Mwaka 2002 walipotwaa Kombe la Dunia kwa mara ya mwisho na hiyo ikiwa mara ya 5 katika Historia yao.
Lakini kipigo hicho cha Germany, kikiwa mara ya kwanza kwa Brazil kufungwa Nyumbani kwao katika Miaka 39, kiliwauma sana Wabrazil.
Kwenye Mechi hiyo na Germany, Brazil walimkosa Staa wao Neymar alieumizwa kwenye Robo Fainali na pia kumkosa Nahodha wao Thiago Silva aliekuwa kafungiwa Mechi moja.
Mara baada ya Mechi hiyo na Germany, ambayo walipigwa Bao 5 ndani ya Dakika 29 za kwanza na Bao la Pili hadi la 5 kufungwa ndani ya Dakika 6 tu, Scolari alitamka: “Nitakumbukwa kama Kocha niliefungwa 7-1 lakini nilijua hatari hii nilipochukua kazi hii! Mtu anaepanga Timu, mbinu, ni mimi. Ni chaguo langu!”

No comments:

Post a Comment