EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, March 6, 2014

TANZANIA YAINGIZA TIMU 20 MICHUANO YA KUNG-FU ZA KICHINA



NA: MSHAMU NGONJWIKE……….Dr es salaam
TIMU 20 zinatarajiwa kushiriki mashindano ya Kung Fu  ya Kichina  yatakayofanyika kuanzia Juni 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na SWACOTZ FORUM jijini Dar es Salaam,  Mwenyekiti wa Taifa wa mchezo huo Mwarani Mutee alisema mashindano hayo yatawahusu wanachama wao ambao ni hai ambao ndi watakaoruhusiwa kushiriki.
“Tunategemea kufanya mashindano makubwa Juni 6  Dar es Salaa, timu 20 zinatarajiwa kushiriki katika mashindani hayo.
“Watakaoruhusiwa kushiriki mashindano hayo ni wale wanachama ambao ni hai wanaofuata taratibu na kanuni zetu,” alisema.
Alisema lengo la mashindano hayo ni kuhakikisha mchezo huo unakuwa maarufu kwa wapenda kama ilivyo michezo mingine, kudumisha undugu na kuwaleta watu pamoja.
“Lengo kubwa ni kuhakikisha mchezo wetu unakuwa maarufu kama ilivyo michezo mingine, pia kuwaleta wanamichezo pamoja na kubadilishana mawazo,” alisema.

No comments:

Post a Comment