EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, March 6, 2014

MAGEREZA KUKIPIGA JUMAPILI HII



NA MSHAMU NGOJWIKE……..Dar es salaam
TIMU ya mpira wa Magongo ya Magereza Ukonga inatarajiwa kushuka dimbani Jumapili wiki hii  kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Dar es Salaam Institute (DI) ikiwa ni moja wa maandalizi yao ya mashindano ya klabu bingwa ya Muunguano.
Akizungumza na SWACOTZ FORUM jijini Dar es Salaam jana, kocha mkuu wa timu hiyo Merika Kahola alisema kuwa mechi hiyo itakuwa ya kwanza katika orodha yao ya mechi za kirafiki kabla ya kuanza michuano hiyo.
Alisema kuwa mchezo huo utakuwa ni moja ya kipimo kwa kikosi chake kinachojiandaa na michuano ya klabu bingwa ya Muungano inayotarajiwa kuanza Machi 14 hadi 17 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kahola alisema kuwa baada ya mechi hiyo timu yake itakuwa na mechi nyingine ya kujipima nguvu dhidi ya timu ya Dar Kalsa ambayo watapanga ni lini watacheza mechi hiyo.
“Tumeshafanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya michuano ya klabu Bingwa ya Muungano, hiyo kwa sasa tutacheza mechi kadhaa za kirafiki kabla ya kuingia kwenye michuano hiyo rasmi ambapo kwa kuanzia Jumapili tutacheza na Dar es Salaam Institute kwenye Uwanja wetu wa magereza” alisema.
Alisema kuwa baada ya kutwaa ubingwa wa kombe la miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar sasa anakiandaa kikosi chake kwa ajili ya kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment