EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Tuesday, February 25, 2014

ENZO ZIDANE AIKANA SPAIN KUICHEZEA FRANCE U-19!

ENZO_ZIDANEKOCHA wa Timu ya Vijana ya Real Madrid, Willy Sagnol, amethibitisha kuwa Mtoto wa Lejendari Zinedine Zidane ameitwa kwa mara ya kwanza kuichezea Timu ya Taifa ya France ya Vijana wa chini ya Miaka 19, U-19.
Enzo Zidane, mwenye Miaka 18, alizaliwa France lakini akachukua Uraia wa Spain Mwaka 2006 na Mwaka 2009 aliitwa kuichezea Spain U-15.
Shirikisho la Soka la France, FFF, limethibitisha kuwa Kijana huyo atajiunga Kambi ya Mazoezi ya France U-19 huko Clairefontaine Wiki ijayo.
Willy Sagnola amesema: “Mchezaji ameamua kuvaa Jezi ya Bluu kwa sasa. Baadae anaweza kubadilika lakini nia yake ni kuichezea France.”
Enzo Zidane anaweza kuamua kuzichezea Nchi za Spain, France na hata Algeria wanakotoka Babu zake atakapoamua kwani Mechi za Kirafiki, kwa mujibu wa Kanuni za FIFA, hazimfungi Mchezaji kucheza Mashindano rasmi Nchi hiyo hiyo aliyovalia Jezi.
Mtoto huyo wa Zinedine Zidane, ambae sasa ni Kocha Msaidizi wa Real Madrid chini ya Carlo Ancelotti, alijiunga na Timu za Vijana za Real Madrid tangu 2004.
Enzo Zidane ni mmoja wa Watoto wa Kiume wanne wa Zidane na Mama yao Veronique Fernández wengine wakiwa ni Luca, Theo, na Elyaz, na wote huchezea Timu za Vijana za Real Madrid za Marika tofauti.

No comments:

Post a Comment