EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, February 13, 2014

AS ROMA YABAMIZWA NA NAPOLI COPPA ITALIA


COPPA_ITALIA_2014BAADA kufungwa 3-2 kwenye Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya Coppa Italia, Napoli Jana Usiku ilishusha kipigo kizuri kwa AS Roma walipoitandika Bao 3-0 na kutinga Fainali watakayocheza na Fiorentina.
Juzi, Fiorentina ilitinga Fainali baada ya kuibwaga Udinese Bao 2-0 na kusonga kwa Jumla ya Bao 3-2.
Katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali, Udinese ilishinda Bao 2-1.
Huku wakishuhudiwa na Nguli wa Argentina, Diego Maradona, aliewahi kuwapa mafanikio makubwa alipochezea Klabu hiyo, Napoli hawakumsaliti na kuichapa AS Roma Bao 3-0 kwa Bao za Callejon, Dakika ya 33, Higuain, 48, na Jorginho, 51.
AS Roma walimaliza Mechi hii Mtu 10 baada Strootman kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 79 kufuatia Kadi za Njano mbili.
Napoli wamesonga Fainali kwa Jumla ya Mabao 5-3.
VIKOSI:
Napoli: Reina; Maggio, Fernandez, Albiol, Ghoulam; Inler, Jorginho (Henrique 85); Mertens, Hamsik (Behrami 76), Callejon; Higuain (Insigne 82)
AS Roma: De Sanctis; Torosidis (Maicon 49), Benatia, Castan, Bastos; Pjanic (Totti 61), De Rossi, Strootman; Ljajic (Florenzi 55), Destro, Gervinho
COPPA ITALIA
RATIBA:
FAINALI
Mei 3
Fiorentina v Napoli

No comments:

Post a Comment