EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Sunday, January 19, 2014

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KUFUATIA KIFO CHA MKE WA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Jaji Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mheshimiwa Damian Zefrin Lubuva kufuatia kifo cha Mke wake, Mama Martha Peter Lubuva kilichotokea tarehe 17 Januari, 2014 katika Hospitali ya Apollo iliyoko New Delhi nchini India alikopelekwa kwa matibabu akisumbuliwa na ugonjwa wa Kisukari.
“Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa za kifo cha Mke wako, Mama Martha Peter Lubuva aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Apollo nchini India akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Kisukari ambao umesumbua kwa muda mrefu”, amesema Rais Kikwete katika salamu zake za Rambirambi.
Rais Kikwete amesema anatambua fika machungu ambayo hivi sasa wanapitia watoto na Familia nzima ya Mheshimiwa Damian Zefrin Lubuva kutokana na kuondokewa na Mama yao Mzazi na Kiongozi
muhimu wa Familia, lakini amewaomba wawe watulivu na wavumilivu, lakini muhimu zaidi wawe na moyo wa ujasiri katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya mpendwa wao.
“Ninawahakikishia kuwa niko pamoja nayi katika kuomboleza msiba huu mkubwa na namuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aipokee na kuilaza Mahala Pema Peponi Roho ya Marehemu, Mama Martha Peter Lubuva kwa kutambua kuwa yote ni Mapenzi yake Mola”.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
DAR ES SALAAM.
18 Januari, 2014

No comments:

Post a Comment