EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, January 30, 2014

MHADHIRI WA CHUO KIKUU ATIWA MBARONI KWA KOSA LA KUZUNGUMZA KISWAHILI KWENY NDEGE



ALIYEKUWA Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Azavel Lwaitama, amejikuta akipelekwa polisi baada ya kutokuwa tayari kuzungumza lugha ya Kiingereza ndani ya ndege ya Precision Air. Dk. Lwaitama alikutana na dhahama hilo juzi alipokuwa safarini akitokea Dar es Salaam kwenda mkoani Kagera, kabla ya kufika Bukoba ndege aliyopanda msomi huyo ilitua jijini Mwanza.
Akiwa jijini hapo, alipanda ndege ya kuelekea Bukoba ya kampuni ileile iliyomtoa jijini Dar es Salaam, yenye namba za usajili PW 0492, ambapo alitakiwa kukaa kiti namba 2B.

Kilipo kiti hicho ndipo palipo na milango ya dharura kwa pande zote mbili za ndege, ambapo alikwenda mhudumu wa ndege hiyo na kumuuliza kama anajua kuzungumza Kiingereza.


Hata hivyo, Dk. Lwaitwama inadaiwa kuwa alimfanyia mzaha mzaha wa kawaida kwa kumuuliza kama ni lazima ajue Kiingereza.

Baada ya mzaha huo, mhudumu huyo alimwambia kama hajui lugha hiyo basi ahame kiti na kukaa sehemu nyingine kwani kuna maelezo rasmi ambayo yanatolewa kwa "lugha ya anga" ambayo ni Kiingereza, hivyo abiria anayepaswa kukaa hapo ni lazima ajue lugha hiyo.

Dk. Lwaitama alihoji ni kwanini lugha ya anga isiwe inayoeleweka na abiria wengi na kwamba katika ndege nyingi alizosafiri nazo kote duniani, lugha za anga huwa zile za wasafiri wengi wa eneo husika na lugha nyingine za kimataifa.

Mhudumu huyo hakuridhika na majibu hayo na kuamua kumuita mwenzake na wote wawili walikimbilia kwa rubani kushitaki kuwa kuna mtu "anafanya fujo."

Alichokifanya rubani ni kumwambia msomi huyo kuwa hawezi kusafiri na kuwaita polisi ambao walimtoa nje ya ndege.

Baada ya hali hiyo, alitakiwa kutoa maelezo na baadaye kuwekewa dhamana, ambapo anatakiwa kuripoti tena polisi keshokutwa.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani hapa, Joseph Konyo amesema kuwa ni kweli tukio hilo limetokea na kwamba uchunguzi unaendelea ambapo, Dk. Lwaitama anatakiwa kuripoti polisi siku ya Ijumaa.

>>MTANZANIA

No comments:

Post a Comment