NA: /Mohamedi,Zawadi & Majidu.
Wafanyabiashara wa
Soko la Kiyangu mkoani Mtwara wameiomba serikali kuboresha na kuweka
huduma muhimu katika soko hilo, ikiwepo pamoja na huduma ya choo, maji, umeme
na usafi.
Hayo yamesemwa
mapema hii leo na wafanyabiashara wa soko hilo wakati wakizungumza na
Mwandishi wa Habari wa Pride Fm Redio, walipokuwa wanatoa kero zao kuhusiana na soko hilo.
Mmoja wa wafanyabiashara hao Bi Somoe Hamisi,
amesema kuwa kumekuwepo na tatizo la ukosefu wa choo kwa muda mrefu katika soko
hilo ,ambapo inapelekea wafanyabiashara hao kujisaidia katika maeneo ya soko hali
ambayo inahatarisha afya zao.
Aidha Bi Asha Bakari na Dayness Muhaja wametaja
matatizo mengine kuwa ni pamoja na
ukosefu wa umeme na maji katika soko hilo kongwe, na kulalamikia hali ya usafi
kuwa ni mbaya na kupelekea wafanyabiashara wengi kuhamia katika masoko mengine.
Wafanyabishara hao wametoa wito kwa serikali na
uongozi wa Manispaa kushughulikia kwa haraka tatizo la ukosefu wa choo ili
kunusuru afya zao pamoja na wateja wa bidhaa katika soko hilo.
No comments:
Post a Comment