EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Saturday, November 2, 2013

NEUER KIPA PEKEE KATIKA ORODHA YA WATAKAOGOMBEA BALLON D'OR.

GOLIKIPA nyota wa klabu ya Bayern Munich, Manuel Neuer amesema amefurahishwa kuwa golikipa pekee kuchaguliwa kugombea tuzo ya mchezaji bora wa dunia maarufu kama Ballon d’Or mwaka huu. Neuer ni mmoja kati ya wachezaji sita wa Bayern walioingia katika orodha hiyo ya wachezaji 23 baada ya timu hiyo kufanikiwa kushinda mataji matatu mfululizo katika msimu wa 2012-2013. Akihojiwa Neuer amesema ni heshima kubwa kwake kuwa golikipa pekee aliyepata nafasi hiyo na wote wanategemea kwamba mchezaji mojawapo katika Bayern ndiye atakayeibuka kidedea katika tuzo hizo. Bayern ambayo msimu uliopita ilikuwa ikinolewa na Heynckes, imeendelea kuwa katika kiwango cha juu chini ya kocha mpya Pep Guardiola toka kuanza kwa msimu mpya na Neuer ameeleza kufurahishwa na jinsi wanavyocheza hivi sasa.

No comments:

Post a Comment