EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Saturday, October 19, 2013

WAZIRI MKUU ATAKA TAASISI ZA MAFUNZO YA UONGOZI CHINA NA TANZANIA KUANDAA KOZI KWA VIONGOZI



Waziri  Mkuu Mizengo Pinda amesema kuna haja ya taasisi za mafunzo ya uongozi za China na Tanzania kuandaa kozi zenye kuwafaa makundi fulani ya viongozi ambazo zitasaidia kubadili mwelekeo wao na utendaji kazi hasa katika masuala yanayohusu sekta binafsi.
waziri mkuu wa Tanzania-MH:Mizengo Pinda
=Alimesema taasisi hizo zinapaswa kuwa na uelewa mkubwa kuhusu ushirikiano wa pamoja baina ya sekta binafsi na za umma (PPP), zinapaswa kujua faida za ushirikiano huo na zinapaswa kubainisha ni sekta zipi zinapaswa kutekeleza mpango huo wa ushirikiano. Alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua mafunzo ya siku 14 kwa maafisa 20 kutoka idara na taasisi za serikali ya Tanzania yanayoendeshwa kwa pamoja baina ya Chuo cha Uongozi cha China na Taasisi ya Uongozi ya Tanzania.


 Mafunzo hayo ni sehemu ya mpango wa Serikali kuboresha utendaji wa  Maeneo ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZ) yaliyoanza jana kwenye Chuo cha Uongozi cha China (China Governance Academy),  jijini Beijing, China.
Alisema Tanzania imefanya maamuzi ya kutumia ushirikiano wa pamoja baina ya sekta binafsi na za umma (PPP) kama njia ya kukuza na kuendeleza miundombinu, kuhamisha ujuzi na teknolojia pamoja na ujenzi wa viwanda.
“Ni muhimu taasisi zetu hizi mbili zikatambua jambo hili na kuchangia kwa juhudi zote ili kuhakikisha kuwa linafanikiwa,” alisema.
Alisema kozi kama hizo zinapaswa kuwalenga watumishi kutoka taasisi za serikali pamoja na sekta binafsi na akazitaka taasisi hizo kuhakikisha zinasaidia kuwepo kwa ufanisi wa hali ya juu kwenye ushirikiano wa pamoja baina ya sekta binafsi na za umma.
“Muwasaidie watu hawa waweze kutambua ni wakati gani ushirikiano wa aina hii unakuwa wa manufaa zaidi kwa wahusika, ni wakati gani wahusika wanafaidika na PPP, je wanakabiliwa na changamoto zipi, na wanafanyaje ili kukabiliana na changamoto zinazojitokeza,” aliongeza.
Alisema jambo lililo wazi kuwa ushirikiano baina ya wajasiriamali wa Kichina na wa Kitanzania utasaidia kuongeza fursa za kuhamisha ujuzi na teknolojia pamoja na kuendeleza miundombinu.


“Natambua kwamba kuna wafanyabiashara zaidi ya 500 wa kutoka China ambao wako nchini Tanzania, hawa wanachangia maendeleo ya kiuchumi Tanzania kwa kuingiza teknolojia mpya na kutoa fursa za ajira,” aliongeza.
Waziri Mkuu ambaye yuko katika siku ya tatu ya ziara ya siku tisa ya kikazi kwa mwaliko wa Serikali ya nchi hiyo, alitembelea kiwanda cha aluminium cha China (CHINALCO) na kiwanda cha kutengeneza zana za kijeshi ambako alionyeshwa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na viwanda hivyo.



No comments:

Post a Comment