EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Friday, October 18, 2013

JAM WEEZY TOKA MTWARA ATANGAZA VITA NA BONGO FRAVOUR

JAM WEEEZY msanii wa bongo freva anayekuja
MSANII Juma Omary maarufu kama JAM WEEZY mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa mkoani mtwara ameiambia Swacotz forum kuwa yuko mbioni kuachia ngoma yake mpya itakayojulikana kwa jina la harakati,nyimbo ambayo amesema anatarajia kuifanya kwenye studio za Suri hapahapa mjini mtwara katika maelezo yake Jam Weezy ambaye ametamba mkoani mtwara na nyimbo ya CHAPCHAP aliyoimba na wasanii wenzake wa kundi la NON DISPEAR la mkoani humu pamoja na kushirikishwa kayika nyimbo ya msanii wa musiki aina ya RAGGER DOT KADIO nyimbo iitwayo SPEED amesema kwa sasa amejipanga na ameamua kufanya muziki hivyo wasanii wengine waliotangulia wakae mkao wa vita dhidi yake kwani tayari amekwishaandika mashairi mengi sana mazuri na anaamini akiyaingiza sokoni yatafanya vizuri. licha ya msanii huyo kuwa na nyimbo chache lakini amekuwa ni msanii anayekubalika sana mkoani mtwara huku nyimbo zanazosikika sauti yake zikipendwa na vituo vyote vya radio vilivyopo mkoani hapa mwisho Jam weezy amemaliza kwakuwataka watanzania wote wampokee na kumpa sapoti ya kutosha katika kazi zae.

No comments:

Post a Comment