EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Monday, October 14, 2013

UFARANSA YAJIPANGA KUONGEZA MAJESHI ZAIDI AFRIKA YA KATI



Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ufaransa amesema kuwa, Paris ina mpango wa kuongeza idadi ya wanajeshi wake katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.  
waziri wa mambo ya nje ufaransa
Laurent Fabius ameeleza kuwa, operesheni hiyo ya kupelekwa wanajeshi zaidi wa Ufaransa nchini humo, itaendelea hadi mwishoni mwa mwaka huu wa 2013.Fabius amesema kuwa, mshauri wa Umoja wa Ulaya tayari ameshawasili Bangui mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa shabaha ya kufanya mazungumzo yenye lengo la kuchukuliwa hatua zaidi za kukabiliana na waasi nchini humo.Naye Kristalina Ivanova Georgieva  mshauri wa Umoja wa Ulaya amesema kuwa, hali ya mambo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ni tata mno na karibu wananchi wote wa nchi hiyo wanaathiriwa na machafuko yanayoendelea  nchini humo.
Hadi sasa Ufaransa imeshapeleka zaidi ya wanajeshi 500 katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

No comments:

Post a Comment