EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Monday, October 14, 2013

SHIRIKA LA HAKI ZA BINADAMU LAMKANDAMIZA KENYATA ICC



Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International limesikitishwa vikali, na takwa lililotolewa na Umoja wa Afrika la kuitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, iakhirishe kesi zinazowakabili viongozi wa Kenya. 
 
mwndesha mashtaka mkuu Icc.Fatuo Bensuda

Tawanda Hondora Mkurugenzi Msaidizi wa Sheria na Siasa wa Amnesty International amesema kuwa, taarifa  iliyotolewa na  Umoja wa Afrika, haikuwa sahihi kwani wanasiasa wa bara la Afrika, wanajali maslahi yao na kukanyaga haki za wahanga wa jinai za kivita, jinai dhidi ya binadamu na wahanga wa mauaji ya halaiki.Amesema kuwa, Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto wanakabiliwa na tuhuma uchochezi, mara baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007, zilizosababisha watu wasiopungua 1,500 kuuawa nchini humo. Hondora amesisitiza kuwa, takwa la kusimamishwa kesi inayowakabili Kenyatta na Ruto ni ujumbe wa wazi kwamba, wahanga wa machafuko ya baada ya uchaguzi hawana thamani yoyote ile.

No comments:

Post a Comment