EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Friday, October 18, 2013

TAMASHA LA NGOMA ZA ASILI KWA MAKABILA YA MKOA WA MTWARA YAJULIKANAYO KAMA MAKUYA HATIMAYE YAMEZINDULIWA RASMI HII LEO KATIKA UWANJA WA NANGWANDA SIJAONA MJINI MTWARA.




Tamasha hilo linaloshirikisha makabila matatu maarufu toka mkoani mtwara yaani WAMAKUA,WAYAO na WAMAKONDE limezinduliwa rasmi hii leo katika uwanja wa nangwanda sijaona mjini mtwara ikiwa ni siku ya kwanza ya maonyesho hayo ambayo yatadumu kwa muda wa siku tatu toka kuanza kwake hii leo.
 
Picha mbalimbali za tamasha la MAKUYA
Uzinduzi hu ulioanza majira ya saa nne asubuhi na kumalizika saa kumi na mbili jioni ulihusisha maonyesho mbalimbali ya sanaa za ngoma toka kwa vikundi vya ngoma vya makabila husika ambapo makundi yaliyopata fursa ya kuonyesha michezo yao leo ni kundi la Chipapayungu la kabila la kimakonde,Sinzia toka kabila la wamakua Madudu pia toka kwa wamakonde Mselemba toka katika kabila la wayao.
mshiriki wa tamasha


 Pia michezo kadhaa ilihusika kusindikiza uzinduzi huo michezo hiyo ni kama vile Kulenga shabaha kwa kutumia Mshale,pamoja na kulenga shabaha kwa kutumia manati. Tamasha hilo limeandaliwa na ubalozi wa Finland nchini kwa kushirikiana na makampuni ya DCOs na ADEA ambapo hapo kesho tamasha hilo litaendelea huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa barozi wa Finland  Bibi Sinikka Antila.Ambapo ratiba ya sherehe hizo itaanza saa  mapema asubuhi kwa maandamano yatakayoanzia mnarani mpaka bima na hatimaye nangwanda.
 

No comments:

Post a Comment