EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Friday, October 18, 2013

MAANDALIZI YA MICHUANO YA VYUO VYA UALIMU KANDA YA KUSINI (UMISAVUTA) YAFIKIA HATUA YA MWISHO



michuano inayovikutanisha vyuo vya ualimu kanda ya kusini maalufu kama umisavuta ambayo itaanza kutimua vumbi siku ya jumatatuya tarehe 21 october 2013 katika viwanja vya chuo cha ualimu masandube na chuo cha ualimu mtwara kawaida ttc,
UWANJA WA MICHEZO WA CHUO

 hatimaye maandalizi yake yamefikia tamati na huku chuo cha ualimu masandube ambacho ni mwenyeji wa mashindano hayo kikielezea kuridhika na hali ya maandalizi na kuwa wao kama wenyeji wako tayari kwa michuano hiyo itakayochukua takribani wiki moja .



akitoa taarifa ya jumla ya michuano hiyo mwl wa michezo wa chuo cha masandube barnabas mohuvone amesema kuwa vyuo vinavyotarajiwa kushiriki michuano hiyo ni pamoja na chuo cha ualimu kitangari,mtwara kawaida ttc,nachingwea, songea na masandube yenyewe.
huku akitanabaisha michezo itakayovurumishwa katika michuano hiyo ambapo kwa upande wa mpira kutakuwa na mpira wa miguu kwa wavulana,basket ball,volleybal,na netball.
pia kutakuwa na mbio fupi za mita 100,200,400,na 800 huku mbio za kati zikiwa ni za mita 1500. na katika michezo ya mitupo watahusisha mitupo ya kisahani,kurusha mkuki, pamoja na kurusha tufe. na mwisho kabisa ni mchezo wa mruko ambapo mwaka huu kuna aina moja tu ya mruko nao ni mruko wa chin.

No comments:

Post a Comment