EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Friday, October 18, 2013

WALIMU MKOANI MTWARA WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA WAZAZI



Wazazi na walezi katika Manispaa ya Mtwara Mikindani wametakiwa kujenga mazoea ya kuwapeleka watoto wao kliniki kila tarehe husika  inapofikia, ili kujua ukuaji na mabadiliko ya watoto wao.
wanafunzi wakiwa ktk foleni ya uji

Hayo yameelezwa na mtumishi wa zahanati ya Polisi Ligula nesi Moshi Ahmed wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa pride fm katika zahanati hiyo, ambapo amesema kuwa kwa kuwapeleka watoto kliniki kila awamu itasaidia kujua mabadiliko ya afya ya watoto hao, jukumu ambalo linatakiwa lifanywe kwa ushirikiano kati ya wazazi wa pande zote baba na mama.




Kwa upande wake mmoja wa mzazi Monika Hamisi amesema kuwa kwa wale wazazi wenye imani potofu na kliniki ni kwenda kinyume na malezi na haki ya mtoto, kwani kwa kwenda kilinik kutamwezesha mtoto kupimwa uzito, kwa kujua ongezeko na upungufu wa uzito wa watoto na itasaidia kupunguza tatizo la kupewa dawa tofauti na vipimo pindi atakapoumwa.
Mama Monika ameiomba serikali iongeze kliniki za akina mama na watoto katika maeneo ya vijijini kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kupunguza safari ndefu wanazotumia akina mama kutembea kutafuta huduma za afya ya mama na mtoto.

No comments:

Post a Comment