EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, October 31, 2013

JOE HART NJIA PANDA, KUANZA KIKOSI CHA CITY KATIKA MECHI YA LIGI J'MOSI



JOE_HARTBOSI wa Manchester City Manuel Pellegrini yuko njia panda nani amuanzishe Golini kwenye Mechi yao ya Ligi Kuu England Jumamosi na Norwich City baada Kipa wa Akiba Costel Pantilimon kudaka vizuri mno kwenye Mechi yao ya Jumatano ya CAPITAL ONE CUP ambayo waliifunga Newcastle Bao 2-0 kwenye Mechi iliyochezwa Dakika 120 baada kutoka 0-0 katika Dakika 90.
Katika Mechi hiyo, Pantilimon, anaetoka Romania, aliokoa Bao mbili na kuiwezesha Man City itoke kwenye Mechi bila kufungwa Bao katika Mechi ya kwanza baada ya Mechi 7.
Joe Hart ndie Kipa Nambari Wani wa Man City  lakini Kipa huyo ambae pia ni Nambari Wani kwa England amekuwa akifanya kosa baada ya kosa katika Mechi zake Msimu huu.
Na Pellegrini ametamka: “Kipa yeyote atakaecheza atakuwa na sapoti yangu. Costel kawaida anacheza Mechi za Makombe ya Ligi na FA na Mechi na Newcastle ilikuwa muhimu kwake.”
Alipobanwa aweke waziwazi nani atakuwa Kipa Jumamosi, Pellegrini alijibu: “Nimeshakwambia nitafikiria hilo Alhamisi.”

No comments:

Post a Comment