EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Tuesday, October 15, 2013

CCM MTWARA YATOA TAMKO ZITO KUHUSU KOROSHO



HALMASHAURI kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mtwara, imetoa wito kwa serikali kuwa makini na kufuatilia kwa ukaribu uendeshaji wa zoezi la ununuzi wa zao la korosho msimu huu, ili kuhakikisha kero za msimu uliopita hazijirudii.
wanachama wa ccm mtwara

Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mtwara Shaibu Akwilombe wakati akitoa maazimio ya mkutano mkuu wa chama hicho, ambapo amesema kuwa hali hiyo ikitekelezwa itapunguza kama sio kumaliza kabisa mianya inayopelekea dhulma na uporaji wa jasho la mkulima mnyonge wa zao la korosho mkoani humo.
Amesema ni wakati sasa kwa wananchi hususani wakulima wa zao la korosho mkoani Mtwara kuhakikisha wanakuwa macho na makini, ili haki zao na maslahi yao kutoporwa na wajanja wachache wanajipandikiza katika biashara ya zao hilo mkoani Mtwara.
Hali hiyo imejiri kufuatia maandalizi ya ununuzi wa zao la korosho kwa msimu wa mwaka 2013/14 kwa sehemu kubwa kushindwa kutoa kuthjoa ufafanuzi wa matatizo ya zao hilo yaliyojitokeza katika msimu uliopita wa 2012/13, yakiwemo ya kushindwa kwa namna bora, sahihi nay a haraka ya ulipwaji wa madeni ya wakulima na mfumo mbaya wa vyama vya ushirika kukopa katika mabenki fedha za kununulia magari.

Matatizo mengine ni pamoja na taarifa za ukaguzi kutowekwa wazi kwa wanaushirika, namna gani madeni ya malipo ya pili yatalipwa kwa wakulima na kwa mfumo gani na namna gani viongozi wa ushirika waliohusika na ufujaji wa mali za ushirika watashughulikiwa ili kurejesha imani ya wakulima kwa vyama vyao na serikali yao.

Akwilombe amesema kuwa kufuatia hali hiyo halmashauri kuu ya CCM imeazimia kuwa vyama vya ushirika vya TANECU na MAMCU kwa pamoja viuze korosho zote za wakulima ambazo hazikuuzwa katika msimu uliopita, bodi ya korosho iondoe na kufanya marekebisho ya mwongozo wa mauzo ya korosho uliotolewa Oktoba 2013 na kuundwa kwa tume itaakayoongozwa na mwenyekiti wa CCM Mkoa kwa ajili ya kufuatilia na kuhakiki korosho za wakulima amabazo hazijauzwa.
Maazimio mengine ni serikali ya mkoa ifuatilie na kuhakikisha taarifa za ukaguzi wa mahesabu ya vyama yaliyofanywa mwaka jana, serikali ya mkoa imuombe mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali afike mkoani Mtwara kwa ajili ya ukaguzi na serikali ya mkoa ihakikishe katika msimu huu mkulima analipwa malipo yake yote, ndipo makato yanayotozwa na vyama vya ushirika na halmashauri za wilaya yafanywe.
CONTINUE

No comments:

Post a Comment