EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Tuesday, October 15, 2013

SERIKALI YAUNDA TUME KUCHUNGUZA UFISADI


Naibu waziri wa serekali za mitaa na tawala za mikoa MH:Agrey Mwanri

SERIKALI imeamuru kuundwa kwa tume, ili kuchunguza matumizi ya Sh milioni 324 za mradi wa umwagiliaji wa Golani, mkoani Tanga.
Naibu Waziri wa Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa (TAMISEMI), Agrey Mwanri ametoa agizo hilo mbele ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Benedict Ole Kuyan na kumtaka kuunda tume na kumpelekea taarifa haraka baada ya kutoridhishwa na mradi huo uliopo Kijiji cha Pande “B”.
Mwanri amebaini kuwapo matumizi mabaya ya pesa hizo za miradi yaliyofanywa na Wataalamu wa Idara ya Kilimo ya Jiji wakati alipotembelea mradi huo na kuzungumza na wananchi.
Amesema kuwa fedha zilizotumika kuendesha mradi huo haziendani na hali halisi ya bustani, na kwamba mengi yaliyoandikwa kwenye taarifa hayapo eneo husika.Naibu waziri huyo amesema kuwa kwa mujibu wa taarifa hiyo ilieleza mradi huo unatekelezwa na Halmashauri ya Jiji, lakini alipofika kwa wakulima akaambiwa wanaofanya kazi zote ni wakazi wa kijiji hicho. Mradi mwingine uliopo mkoani Tanga, ambao hakuridhika nao ni ule wa ujenzi wa kituo kipya cha mabasi ya mikoani kilichopo Kange

No comments:

Post a Comment