EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Tuesday, July 16, 2013

KIFAHAMU KIKOSI CHA MSIMU HUU CHA MADRID KILICHOANZA MAZOEZI RASMI HIKI HAPA






ADIDAS YASIMAMISHA MKATABA WAKE WA UDHAMINI NA GAY KWASABABU YA MADAWA.

KAMPUNI ya vifaa vya michezo ya Adidas imesimamisha mkataba wake wa udhamini na mwanariadha nyota wa mbio fupi Tyson Gay wa Marekani baada ya kukutwa na chembechembe za dawa za kuongeza nguvu. Msemaji wa kampuni alidai kuwa awameshtushwa na tuhuma hizo kwa Gay na hata kama bado hajakutwa na hatia ya kosa hilo moja kwa moja kampuni itasimamisha udhamini wake mpaka hapo hukumu itakapotolewa. Gay mwenye umri wa miaka 30, ndio mwanariadha wa pili mwenye kasi zaidi duniani katika mbio za mita 100 akiwa sambamba na Yohan Blake wa Jamaica na pia ndiye mwanariadha aliyeweka rekodi ya kasi zaidi kwa mwaka huu. Nyota huyo ambaye aliwahi kuwa bingwa wa dunia katika mbio za mita 100, 200 na mita 400 kupokezana vijiti mwaka 2007 alishindwa kukata tuhuma hizo na kudai kuwa alimwamini mtu ambaye alimwangusha na hivyo atapokea adhabu yoyote atakayopewa.

MADRID YAIPIGA KIKUMBO MAN UNITED KATIKA ORODHA YA VILABU TAJIRI DUNIANI.

KLABU ya Real Madrid ya Hispania imetajwa kuwa klabu yenye thamani zaidi katika orodha ya timu za michezo 50 zenye thamani zaidi duniani iliyotolewa na jarida Forbes la nchini Marekani. Katika orodha hizo timu za Ligi Kuu ya Mpira wa Kimarekani-NFL ndizo zilizoonekana kutawala kwa kiasi kikubwa. Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na jarida hilo Madrid ambao ni mabingwa mara tisa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya wana utajiri unaofikia dola bilioni 3.3, utajiri huo ukiwa umeongezeka kwa dola bilioni 1.88 kulinganisha na mwaka uliopita baada ya kuongeza mapato yao kwa kuingia mikataba na kampuni za Adidas na Shirika la Ndege la Emirates. Manchester United wamepigwa kikumbo na Madrid na kushuka mpaka nafasi ya pili wakiwa na utajiri wa dola bilioni 3.17 wakati mabingwa wa Hispania Barcelona wao wamekwea kutoka nafasi ya tano mpaka ya tatu wakiwa na utajiri unaofikia dola bilioni 2.6. Nafasi ya nne inashikiliwa na timu ya Baseball ya Marekani ya New York Yankees ambao wana dola bilioni 2.3, wakifuatiwa na Dallas Cowboys ya NFL dola bilioni 2.1 na New England Patriots dola bilioni 1.6. Nyingine ni Los Angeles Dodgers ya baseball dola bilioni 1.6, timu za NFL Washington Redskins na New York Giant pamoja na klabu ya soka ya Arsenal ya Uingereza ambazo zote hizo zina utajiri wa dola bilioni 1.3.

FENERBAHCE, BESIKTAS ZAGONGA MWAMBA UEFA.

SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya-UEFA, limesema kuwa klabu za Fenerbahce na Besiktas za Uturuki zimeshindwa rufani zao za kupinga adhabu ya kushiriki michuano inayoandaliwa na shirikisho hilo. Fernabahce ambao ilikuwa washiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu walifungiwa kushiriki michuano yoyote ya Ulaya kwa misimu miwili huku Besiktas ambao walifuzu kushiriki michuano ya Europa League wao wamefungiwa msimu mmoja. Klabu zote mbili zinatuhumiwa na kashfa ya upangaji matokeo katika baadhi ya mechi za Ligi ya Kuu ya Soka nchini Uturuki mwaka 2011. Baada ya kugonga mwamba UEFA, klabu hizo bado zina haki ya kukata rufani katika Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo-CAS.

FIFA YAZIDI KUIKOMALIA CAMEROON.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limedai kuwa klabu ya Coton Sport ya Cameroon haitaruhusiwa kucheza mechi yao ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika mwishoni mwa wiki hii kwasababu ya adhabu iliyopewa Shirikisho la Soka la nchi hiyo-Fecafoot na FIFA. Hatua ya kuzuiwa kwa klabu hiyo kunazidi kuleta utata katika michuano hiyo mikubwa kabisa ya vilabu barani Afrika huku mahasimu wa soka nchini Misri klabu ya Zamalek na Al Ahly ambao ndio mabingwa watetezi nao wakiwa hawajui hatma ya mechi baina yao kwasababu ya vrugu za kisiasa zinazoendelea nchini humo. Timu nane zilizofanikiwa kuvuka hatua ya makundi, ndio zinatarajiwa kuchuana kutafuta washindi watakaocheza nusu fainali ya michuano hiyo katika mechi zao za kwanza mwishoni mwa wiki hii. FIFA imesema kuwa tayari wameshaanza mazungumzo kujaribu kutatua mgogoro wa Cameroon lakini mpaka sasa hakuna lolote lililofikiwa mpaka kuwashawishi kuondoa adhabu ya kuifungia nchi hiyo kushiriki michuano yoyote ya kimataifa waliyoitoa Julai 4 mwaka huu. Kufungiwa kwa Cameroon kumekuja kufuatia uchaguzi wa Juni 19 ambao Mohammed Iya alichaguliwa tena kuongoza Fecafoot pamoja na kukamatwa kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha wakati akiongoza kampuni ya Cotton Development Corporation inayomiliki timu ya Cotton Sport. 
Kwa upnde mwingine Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF bado halijateua uwanja utakaotumika kwa ajili ya mchezo wa Zamalek na Al Ahly unaotarajiwa kuchezwa Jumapili kutoka mamlaka za usalama kushindwa kuhakikisha ulinzi jijini Cairo pamoja na mji wa Alexandria kwasababu ya vurugu za kisiasa zinazoendelea.

No comments:

Post a Comment