EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Monday, June 24, 2013

YANGA YAPANGA KUIFUMUA TANZANIA KISOKA SASA INATAKA KUCHEZA KAMA ULAYA

yusuph manji kushoto mw/kt Yanga
Uongozi wa klabu ya soka ya dar young African umesema kuwa wamepanga kufanya kikao kizito na wachezaji wake siku chache zijazo ili kujadili mustakabali wa klaabu hiyo katika kujiandaa kuelekea msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara2013-2014.

www.kassimngumbi.blogspot.com
Lawlenc Mwalusako katibu mkuu Yanga
katibu mkuu wa klabu hiyo Lawlenc Mwalusako amesema kuwa kikao hicho kinatarajiwa kufanyika mapema  mwezi july mara baada ya wachezaji wote kurejea toka mapumzikoni ambapo wanatakiwa kuripoti klabuni hapo siku ya tar moja mwezi ujao na kuanza rasmi mazoezi yao siku ya tar mbili mwezi huohuo july mara baada ya kocha mkuu wa timu hiyo ERnie Brandts kurejea toka nchini kwao Serbia ambakoo yuko kwa sasa kwa mapumziko ya mwisho wa msimu.
Ernie Brandts-kocha mkuu Yanga
katika taarifa yake Mwalusako amesema kuwa kikao hicho kinalenga kinalenga kuzungumzia mikakati na mipango ya klabu yao katika kuhakikisha wanalinda heshima yao na kutetea ubingwa wa Tanzania bara ambao wanaushikilia kwa sasa lakini kuhusiana na tarehe Mwalusako ameeleza kuwa kutapangwa tarehe ya kufanyika kwake mara tu baada ya Brandts kuingia na kutolewa kwa ratiba ya ligi kuu ambayo ndiyo itakuwa ni mwongozo wao kuhusu vitu gani wapange kulingana na mechi watakazopangiwa.
mwalusako kulia







No comments:

Post a Comment