EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Monday, June 24, 2013

TENGA,HOSEA WAWATIBUA WATANZANIA. WADAU WASOKA WADAI WAMEPANGA NJAMA ZA KUIRUBUNI TFF NA STARZ

www.kassimngumbi.blogspot.com
Rais wa TFF Leodiga Chilla Tenga
Chama cha mpira wa miguu nchini TFF kimeonekana kutatanisha na kuwachanganya wananchi na  wadau wa soka la Tanzania kutokana na kauli yake iliyoitoa mapema hapo jana kuwa wamepanga kujadili masuala yahusuyo katiba inayoiongoza chama hicho Tar:13 July siku ambayo timu ya taifa ya Tanzania taifa starz itakuwa ikikipiga na timu ya taifa ya Uganda The Cranes katika mchezo wa kuwania kufudhu kushiriki katika michuano ya Afrika inayoshirikisha  wachezaji wanaoshiriki ligi la ndani.

www.kassimngumbi.blogspot.com
uongoz TFF
kauli hiyo imetolewa na katibu mkuu wa TFF Angetile Hosea Mwalubeja imeonyesha kuamsha hisia za watanzania kwa kutokuwa na imani na upangwji wa ratiba hiyo kwani wanahisi kuwa kuna michezo michafu inataka kufanyika ndani ya TFF kuhusu katiba.Akielezea wasiwasi wake moja kati ya wadau wa soka nchini amadhan Hamisi ama Don King amesema kuwa wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF ambao wanatakiwa kuhudhulia kikao hicho pia ni watu muhimu katika kuhudhulia mechi ya starz na Uganda na ni lazima wafanye hivyo kama sehemu ya majukumu yao hivyo basi kitendo cha mambo haya mawili kufanywa siku moja wao wanaona kama njama ya kuwafanya wajumbe hao washindwe kufanya maamuzi yao sahihi kwani watakuwa na haraka ya kuwahi mchezo pia,kitendo ambacho kitawapa mwanya mafisadi wanaorubuni soka la Tanzania kuingiza mikono yao kwa nia mbaya.

No comments:

Post a Comment