MTOTO MWENYE UMRI ZAIDI YA MIAKA MIWILI AFUNGIWA NDANI ZAIDI YA MIAKA MIWILI NA WAZAZI WAKE IYUNGA JIJINI MBEYA ......RIPOTI KAMILI HII
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtoto mwenye umri wa zaidi ya
miaka miwili amefungiwa ndani na wazazi wake kwa kipindi cha miaka miwili sasa
bila kutoka nje pamoja na kukosa matunzo muhimu hali ambayo imepelekea mtoto
huyo kudhoofu kiafya.
Tukio hilo limetokea leo jijini mbeya
katika mtaa wa Ikuti kata ya Iyunga ambapo majirani wa karibu na mtoto
huyo pamoja na baadhi ya viongozi wa mtaa huo kufika nyumbani anapoishi mtoto
huyo kwa lengo la kufahamu maendeleo yake .
Mtoto huyo amefahamika kwa jina la
Joshua Joseph umri unao kadiriwa kuwa ni kati ya miaka miwili au mitatu
ambaye alikutwa nyumbani hapo akiwa pekee yake huku wazazi wake wakiwa
wameondoka kuelekea kwenye shughuli zao .
Akizungumzia tukio hilo Kaimu barozi
wa mtaa huo wa Ikuti Ndugu Aloni Mboya amesema kuwa hali hiyo imenza kujitokeza
kwa kipindi cha miaka mitatu sasa hali ambayo imepelekea mtoto huyo kukumbwa na
maradhi ya utapiamlo.
Amesema katika kipindi cha mwaka 2011
mwezi wa tatu alipokea taarifa kuhusiana na suala hilo
ambapo baba wa mtoto huyo ndugu Joseph Simoni aliitwa katika ofisi za
mtaa kwa lengo la kumhoji juu ya malezi ya mtoto huyo.
Aidha baada ya kuhojiwa alikiri
kosa ambapo alipewa onyo na viongozi wa mtaa ambao walimtaka kuhakikisha anamtunza
vema mtoto huyo kwa kumpatia chakula bora pamoja na huduma nyingine.
Mara baada ya mtu huyo kupewa kalipio
na viongozi wa mtaa hali hiyo iliendelea tena ambapo wao kama viongozi wa shina
pamoja na wananchi walimuita yeye pamoja na mke wake aitwaye Sekera
Watsoni (40) kuhama mtaani hapo kwa kwa kipindi cha miezi sita ambapo walikaidi
agizo hilo.
Amesema mara baada ya watu hao
kugoma waliamua kuwaacha na kuwaondoa katika umoja wa ubarozi wao na kuto
watambua tena kama wananchi wa eneo hilo kutokana na vitendo vyao vya kikatili
dhidi ya mtoto huyo.
No comments:
Post a Comment