EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, May 23, 2013

Gas City: Wanasiasa waaswa kutochochea vurugu

Gas City: Wanasiasa waaswa kutochochea vurugu

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila akifunga kikao cha bodi ya Barabara Mkoa
Naibu Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa [TAMISEMI] Kassim Majaliwa ambaye ni mbunge wa Ruangwa amewataka wanasiasa mkoani Lindi kuacha tabia ya kuwa chanzo cha kuchochea vurugu katika jamii badala yake washirikiane na watendaji na wananchi ili kuinua mkoa huo ambao uko nyuma kimaendeleo.
Naibu waziri wa Nchi Twala za Mikoa na Serikali za Mitaa ambae ni Mbunge wa jimbo la Ruangwa akibadilishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Dr Nassor Ally Hamid wakati wa mapumziko
mafupi ya Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Lindi.
Naibu waziri huyo ametoa wito huo wakati anazungumza na wajumbe wa kikao cha kamati ya ushauri mkoa [RCC] katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Lindi. 
Amesema kuwa, kazi kubwa ya wanasiasa ni kutembelea wananchi kwa lengo la kuwasikiliza kero zao, kuwahimiza na kuwahamasisha wananchi katika maeneo yao ili kuchochea maendeleo na sio kuchochea kufanya vurugu na kusababisha kuvunjika kwa amani.

Wenyeviti wa Halmashauri za mkoa wa Lindi wasikiliza kwa makini kikao cha Bodi ya Barabara

Wakuu wa wilaya za mkoa wa Lindi
Wanasiasa wamekuwa na nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko chanya katika maeneo yao kwa kuhamasisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo badala ya kushiriki vurugu.
“sio vyema wanasiasa waliochaguliwa na wananchi kwa ajili ya kusimamia na kuwawakilisha wakatumia nafasi hiyo majukwaani kutamka maneno ya uchochezi na kusababisha kupotea mwelekeo wa kuwaletea wananchi wake maendeleo hii inaonesha usivyotosha kwa wapiga kura.”

No comments:

Post a Comment