Gas City: Sospeter Muhongo Dodoma, wananchi wa Mtwara majumbani
Wakati mjadala mkali ukitarajiwa kuibuka bungeni leo wakati
Serikali itakapokuwa ikiwasilisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, joto
limezidi kupanda mkoani Mtwara ikielezwa kuwa wananchi wamehamasishana kwa mara
nyingine kuacha shughuli zote ili kusikiliza kama hotuba hiyo italinda masilahi
yao.
![]() |
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo |
Hotuba hiyo ambayo itasomwa leo mara baada ya kipindi cha
maswali na majibu bungeni na Waziri wa wizara hiyo, Profesa Sospeter Muhongo,
inatarajiwa kuibua mengi yakiwamo yanayohusu suala la gesi ya Mtwara.
Mjini Mtwara vipeperushi vinavyopingana vilisambazwa
kuhamasishana ‘kuacha shughuli zao zote na kubaki nyumbani ili kufuatilia
matangazo ya televisheni wakati
Profesa Muhongo atakapotangaza bajeti hiyo, huku vingine
vikipinga.
Ahadi za matumaini
Licha ya kampeni hizo za watu wa Mtwara, Serikali nayo
imeweka matangazo katika vyombo vya habari likiwemo gazeti hili ikieleza namna
mikoa ya Mtwara na Lindi itakavyonufaika na utafutaji na uendelezaji wa Gesi
Asilia.
Tangazo lililotolewa na Shirika la Maendeleo ya Petroli
Tanzania limeainisha faida za gesi hiyo kwa Mkoa wa Mtwara ukiwamo umeme
utakaotokana na gesi asilia. Pia imeelezwa jinsi mafunzo kwa vijana juu ya matatizo
ya gesi asilia yaliyodhaminiwa na Wizara ya Nishati na Madini na kampuni
mbalimbali kuanzia mwaka 2010.
Vilevile imeelezwa jinsi uboreshaji wa huduma za jamii kama
ujenzi wa shule, hospitali na ujenzi wa viwanda kama kile cha saruji cha
Dangote na mitambo ya kusafishia gesi utakavyowanufaisha wakazi wa mkoa huo.
Gesi hiyo ambayo pia inachimbwa katika Kisiwa cha Songosongo
inatajwa kwamba itawanufaisha wakazi wa Mkoa wa Lindi kwa kupata umeme,
kunufaika na kodi ya wawekezaji wa gesi na udhamini wa mafunzo kutoka kampuni
mbalimbali na wizara.
Wiki iliyopita Profesa Muhongo alijigamba kuwa bajeti ya
wizara yake atakayosoma leo itakuwa ya karne ya 22 itakayomaliza tatizo la
umeme nchini kwa kuwa imetoa vipaumbele kwa sekta binafsi kusaidia upatikanaji
wa umeme wa uhakika.
Soma zaidi hapa
Mwalimu wa shule ya msingi kupandishwa kizimbani kwa kumjaza mimba mwanafunzi
Mwalimu wa shule ya msingi kata ya
Msingi tarafa ya Kinampanda wilayani Mkalama Wolter Ponela mwenye umri wa miaka
32, anatarajiwa kupandishwa kizimbani katika mahakama ya wilaya ya Iramba
kujibu tuhuma ya kumjaza mimba mwanafunzi wa kidato cha pili mwenye umri wa
miaka 17.
Mwanafunzi huyo anasoma katika shule ya
sekondari Jerumani iliyopo kata ya Msingi.
Mkuu wa wilaya ya Mkalama Edward Ole
Lenga amesema kuwa, ofisi yake imesikitishwa na kitendo cha mwalimu huyo kwa
madai kuwa kinachangia kuharibu maisha ya msichana husika.
![]() |
Mkuu wa wilaya mpya ya Mkalama
mkoani Singida, Edward Ole Lenga
|
Amesema kuwa, vitendo hivyo ni lazima
vipigwe vita na wadau wote wa elimu ili kuhakikisha wanafunzi wa kike wanasoma
hadi upeo wao bila vikwanzo.
Katika hatua nyingine, mkuu huyo wa
wilaya amekemea vikali tabia iliyoota mizizi ya kumaliza kienyeji matatizo ya
wanafunzi kubebeshwa mimba.
Lenga amesema kuwa, ni lazima sheria
zilizowekwa zitumike katika kukomesha tabia za kuwajaza mimba wanafunzi ambazo
huwa hazitarajiwi au mimba za utotoni.
Aidha, ameagiza watendaji kila mmoja
katika maeneo yake aorodheshe majina ya wanafunzi waliojazwa mimba na watu
waliochangia uharibifu huo wa mimba za utotoni.
Aidha, Lenga amewataka walimu kutenga
muda kuwaelimisha wanafunzi wa kike madhara yatokanayo na mimba za utotoni kama
njia moja wapo itakayosaidia wanafunzi kuchukia vitendo vya mahusiano ya kimapenzi
wakati wakiwa shuleni.
No comments:
Post a Comment