Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad
Maalim Seif alisema hayo alipokuwa akifungua mkutano wa Kanda unaowashirikisha wajumbe kutoka Ethiopia, Mauritius, Kenya, Uganda na Tanzania kujadili usalama magerezani, adhabu mbadala, kutokomeza dawa za kulevya pamoja na maradhi ya Ukimwi uliofanyika mjini Zanzibar.
Alisema kuna kilio kikubwa miongoni mwa mataifa kutokana na kuwapo mazingira yasiyoridhisha katika magereza, hali ambayo imekuwa ni chanzo cha kuvunjwa kwa haki za wafungwa na huchangia watu hao kupata athari za kiafya.
“Dhana yangi ni kuwa nyote mnafahamu hali duni magerezani katika nchi nyingi, hali iliyopo hata vile viwango cha chini vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa kwa haki za wafungwa havifikiwi,” alisema Maalim Seif.
Alieleza kuwa msongamano wa wafungwa na mahabusu katika magereza mengi inachangia kukosekana kwa huduma kama vile kupata mwangaza wa kutosha, hewa safi ambapo matokeo yake kiwango cha maradhi ya kifua kikuu na maambukizi ya ukimwi ni ya kiwango cha juu katika sehemu hizo.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment