Mtu mmoja asiye fahamika jina amefariki dunia April
7 mwaka huu, majira ya saa nne kamili usiku baada ya kupata ajali ya pikipiki,
yenye namba ya usajili T 438 CKJ aina ya SANLG katika kijiji cha maili kumi
barabara ya kutoka Mtwara kuelekea Newala.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mtwara SACP Zelothe
Stephen amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, na kusema kuwa chanzo cha ajali
hiyo ni mwendo kasi ambao umesababisha dereva huyo kuacha barabara na kugonga
kifusi, hivyo kusababisha kupasuka kichwa na kufariki dunia.
Aidha SACP Stephen ameongeza kuwa mwili wa marehemu
huyo umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa
wa Mtwara Ligula na hajafahamika ni mtu wa wapi na jamaa zake bado hawajajitokeza
kuchukua maiti hiyo hadi sasa.
Kufuatia tukio hilo, kamanda huyo ametoa wito kwa
madereva pikipiki kutumia kofia ngumu wanapo endesha pikipiki, ili na kufuata sheria
za usalama barabarani, kwa lengo la kuepusha ajali na vifo visivyo tarajiwa, na
amewaomba wananchi na madereva kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo kwani lipo kwa
ajili ya kulinda raia na mali zao.
MWISHO.
Chanzo-Ajali ya pikipiki.
Repoter Pride Fm, Baraka Jamali.
No comments:
Post a Comment