EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, April 10, 2014

ELIMU LINDI YAKUMBWA NA CHANGAMOTO YA MADAWATI 32,476


Mkuu wa mkoa Lindi Ludovick Mwananzila

Shule za Msingi na Sekondari, mkoani Lindi, zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa madawati, yapatayo 32,476 jambo ambalo linawasababishia idadi kubwa ya wananfunzi kulazimika kusoma wakiwa wameketi sakafuni.
Mkuu wa mkoa Lindi Ludovick Mwananzila ameyabainisha hayo wakati alipokuwa akipokea msaada wa madawati 110 yenye thamani ya Shilingi milioni 20 kutoka mamlaka ya usimamizi wa Bandari Mtwara (TPA).
 Akizungumza na wananchi katika hafla ya kupokea msaada huo, mkuu huyo wa mkoa amesema mahitaji ya madawati kwa mkoa wake ni 68,907 wakati yaliyopo ni 36,431 tu, na kufanya upungufu wa madawati 32,476.
Mwananzila amesema kwa upande wa Shule za msingi kuna upungufu wa madawati 21,988 wakati shule za Sekondari nazo zinakabiliwa na
upungufu wa madawati 10,488.
Amesema Halmashauri ya Lindi vijijini inaoongoza kwa
upungufu wa madawati (6,427), ikifuatiwa na Nachingwea yenye madawati (8,584) na kufanya upungufu (6,904) sawa na asilimia 40.58, Ruangwa mahitaji ni 11,802 lakini yaliyopo ni 9,211 na kufanya pungufu 2,591 sawa na asilimia 31.91.
Mwananzila amesema wilaya ya Kilwa mahitaji ya madawati ni,10,605, yaliyopo ni  (9,026) na kufanya pungufu (1,579) sawa na asilimia 14.89, Liwale ina upungufu wa madawati (1,984) wakati mahitaji ni 7,799 huku yaliyopo 5,815, Manispaa ya Lindi, inayo madawati 3,677 wakati mahitaji ni 6,180 na kufanya upungufu wa madawati 2,503.
                                             MWISHO.
Chanzo, Mwanja Ibadi mwananchi.

No comments:

Post a Comment