KOCHA wa zamani wa timu
ya taifa ya Uingereza, Sven-Goran Eriksson ameiondoa nchi hiyo katika
nafasi ya kunyakuwa Kombe la Dunia litakalofanyika mwakani nchini
Brazil.
Eriksson
mwenye umri wa miaka 65 ambaye sasa ni kocha wa timu ya Guangzhou
R&F inayoshiriki Ligi Kuu nchini China, alioongoza Uingereza kufikia
hatua ya robo fainali katika michuano ya Kombe la Dunia 2002 na 2006.
Akihojiwa
na BBC Eriksson amesema haamini kama Uingereza wanaweza kushinda
michuano hiyo nchini Brazil labda Kombe la Dunia litakalofanyika nchini
Urusi mwaka 2018 kwasababu kuna wachezaji wengi vijana wanaochiukia hivi
sasa.
Uingereza
ambayo inanolewa na Roy Hodgson hivi sasa tayari wameshafuzu kwenda
nchini Brazil mwakani baada ya kuongoza kundi lao lakini katika ratiba
ya michuano hiyo itakayopangwa Desemba mwaka huu Uingereza itakuwa
katika timu za chaguo la pili.
No comments:
Post a Comment