NA : MWANDISHI WETU
Kufuatia maandamano ya waendesha pikipiki maarufu kama
bodaboda wanaofanya shughuli zao katika manispaa ya Mtwara Mikindani Kamanda wa
polisi mkoani Mtwara ACP Zelothe Steven amewataka kutii sheria zilizowekwa na
nchi.
Kamanda Zelothe ameyasema hayo wakati akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake na kueleza kuwa jeshi la polisi halitosita
kumchukulia hatua mtu yeyote atakayevunja sheria kwa kuwa ni wajibu wa kila
mwananchi kutii sheria.
Amesema kutokana na kitendo cha kufunga baadhi ya
barabara na maandamano yaliyofanywa na bodaboda hao hapo jana, ambayo
yalisababisha kero kwa wananchi wengine uamuzi wa jeshi polisi kutuliza ghasia
ulikuwa ni sahihi kwa kuwa ulikuwa ni uvunjaji wa sheria.
Katika Ghasia hizo za jana jeshi hilo limekamata
jumla ya pikipiki 27 zilizotelekezwa na waendeshaji wa pikipiki hizo ambao
walikimbia na watu tisa wanashikiliwa kwa mahojiano zaidi.
Aidha jeshi hilo limewakamata majangili watatu
katika kijiji cha Masuguru wilaya ya Nanyumbu Mkoani Mtwara wakiwa katika
maandalizi ya kwenda katika hifadhi ya Lukwika Lumesule kutekeleza azma ya
kutenda uhalifu.
Watuhumiwa hao walikamatwa silaha mbalimbali ambazo
ni Bunduki aina ya Rifle 458 yenye namba 083972, Risasi 25 za 458, upinde mmoja
na mishale minne, mapanga matatu, silaha nyingine ni visu viwili, tupa mbili,
oil chafu robo lita na vyakula aina mbalimbali na jeshi hilo linaendelea na
msako wa watuhumiwa wengine ambao wamekimbia.
Pia jeshi hilo limemkamata Mtu mmoja anayefahamika
kwa jina la Julius Simon mwenye umri wa miaka 32 katika kijiji cha Lukula Kata
ya masuguru wilayani Nanyumbu akiwa na meno 35 ya Tembo yenye uzito wa
kilogramu 81.8 ambayo thamani yake ni shilingi milioni 451,440,00 swa na tembo kumi na nane waliouwawa.
No comments:
Post a Comment