Tukio hilo limetokea wiki iliyopita muda mfupi baada ya Heche kutoka nyumbani kwake alfajiri kwenda katika kituo cha mabasi ya mikoani cha Ubungo, kuwahi usafiri wa kwenda jijini Mwanza.
Tayari tukio hilo limeripotiwa katika Kituo cha Polisi Mabibo Mwisho na kupewa kumbukumbu namba MAB/RB/225/2014, kabla ya kuhamishiwa katika Kituo cha Polisi Urafiki na kupewa namba URP/RB/2785/2014.
Hata hivyo tukio hilo limeanza kuhusishwa na masuala ya kisiasa hususan katika vitu vinavyodaiwa kuibwa na namna Jeshi la Polisi Kituo cha Urafiki wanavyolishughulikia.
Vitu vilivyoibwa ni pamoja na Friji, radio, TV, Decoder ya Dstv, jezi za mpira jozi 32, mipira 56, magodoro, meza ya TV na music system inayotumika kwenye mikutano ya hadhara.
Hadi sasa tayari mtuhumiwa mmoja anayedaiwa kuhusika na tukio hilo amekamatwa na kukiri kuhusika na tukio hilo pamoja na wenzake ambao bado wanaendelea kusakwa.
“Yule aliyekamatwa amekiri mbele ya Polisi kuhusika na tukio na akawataja wengine sasa tunashangaa kigugumizi cha Polisi katika hili ni nini mpaka wanashindwa kuwafuatilia na kubaini sababu zilizowafanya waibe hapa,” alisema mmoja wa majirani wa Heche.
Kauli ya Heche
Heche ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA alipoulizwa iwapo anaweza kulihusisha tukio hilo na shughuli zake za kisiasa, alisema ni mapema kuhusisha tukio hilo na siasa moja kwa moja.
“Silihusishi moja kwa moja na siasa lakini namna askari wa Kituo cha Polisi Urafiki wanavyolichukulia kiwepesi ndiyo inanipa shaka,” alisema Heche
Kauli ya RPC Wambura
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, ACP Camilius Wambura, alipoulizwa kama analijua tukio hilo alisema hana taarifa nalo na kwamba atafuatilia kujua kama lipo.
No comments:
Post a Comment