EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, April 10, 2014

FILAMU ya Emmanuel Okwi na timu yake ya Yanga inaendelea, sasa ni ukurasa mpya baada ya mchezaji huyo raia wa Uganda kutoa kauli.


Mshambuliaji Emmanuel Okwi.
FILAMU ya Emmanuel Okwi na timu yake ya Yanga inaendelea, sasa ni ukurasa mpya baada ya mchezaji huyo raia wa Uganda kutoa kauli.
Okwi ambaye inadaiwa kuwa amesusa kuichezea timu hiyo kwa kile kilichoelezwa kuwa hajamaliziwa malipo ya fedha zake za usajili, amesema kuwa hawezi kufunguka zaidi kuhusu kinachoendelea.
Lakini amedai kuwa atafanya hivyo mara baada ya timu yake kuivaa Simba, Aprili 19, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya kuzungumzwa mengi kuhusu kususa kwake, Championi Ijumaa lilimtafuta Okwi ambaye hakusema mengi zaidi ya kusisitiza uongozi unajua kinachoendelea na atatoa tamko mara baada ya ligi kukamilika lakini sasa anaendelea na majukumu yake kama kawaida klabuni.
“Siwezi kuzungumza zaidi kwa sasa, kama ni maelezo nitayatoa baada ya mechi ya mwisho ya ligi, kwa sasa kila kitu nimewaachia viongozi,” alisema Okwi na kutotaka maswali zaidi kuhusu kutopangwa na kutokuwepo kwenye kikosi cha Yanga kinachoendelea na mechi za ligi.
Mara baada ya Okwi kutotaka kufunguka zaidi, gazeti hili lilimtafuta rafiki wa karibu wa mchezaji huyo ambaye amekuwa akionekana naye muda mwingi kipindi hiki ambacho yupo nje ya timu, ambaye alisema ni kweli Okwi anaisubiri mechi ya Simba.

“Nasikia Yanga wanasema jamaa ana matatizo ya kifamilia lakini siyo kweli, kama ingekuwa hivyo mimi angeniambia, jamaa (Okwi) hana uhusiano mzuri na baadhi ya viongozi kwa kuwa hawajamkamilishia malipo yake.
“Lakini yeye ukimuuliza anakuwa mgumu kueleza kilicho nyuma ya pazia, tusubiri kuona atakachozungumza, zaidi anachosema ni kuwa anaisubiri mechi hiyo ya Simba,” alisema rafiki huyo ambaye jina lake linawekwa kapuni.
Okwi ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba, alitua klabuni hapo wakati wa dirisha dogo la usajili baada ya kutokea mvutano kati yake na Klabu ya Étoile du Sahel ya Tunisia ambayo ilimsajili ‘bure’ kutoka Simba kisha akatua AS Villa na baadaye Yanga.

No comments:

Post a Comment