EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Saturday, October 12, 2013

MKAPA AIGEUKIA ELIMU TANZANIA KWA UKALI


raisi mstaafu wa awamu ya nne Tanzania MH:Benjamini Mkapa

Kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne mwaka jana kumeelezwa kuchangiwa na mazingira mabovu ya kujifunzia, wanafunzi kutokupenda kujisomea pamoja na uhaba wa vifaa.
Rais Mstaafu Benjamini Mkapa ameyasema hayo jijini Dar es Salaam, wakati akizindua mpango wa usomaji vitabu wenye lengo la kuhamasisha watu kujisomea.
   Mkapa amewalaumu wazazi kwa kutojihusisha na tabia ya usomaji wa vitabu, hali ambayo husababishia watoto wao kuwaiga na kuacha kujisomea vitabu.Amezitaja faida zitokanazo na usomaji vitabu kuwa kumjengea msomaji uelewa mpana wa kufafanua jambo, pamoja na kumpatia fursa mbalimbali za maendeleo.
Zaidi ya asilimia 65 ya wanafunzi walifeli mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, matokeo ambayo yaliilazimu serikali kuunda tume ili kubaini chanzo cha hali hiyo.

No comments:

Post a Comment