NA
MSHAMU NGOJWIKE,
TBF
sasa linaendesha Mashindano ya Klabu bingwa ambayo ilianza kunguruma toka
Aprili 5 hadi 13 mwaka huu kwenye uwanja wa ndani wa taifa,ikishirikisha timu
24.
Akizungumza
na BINGWA jana,Mwenyekiti wa kamati ya
mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania(TBF), Michael Mwita alisema kutokana na
kukosa udhamini katika ligi ya kikapu ya
mwaka huu, ni dalili tosha kwa mchezo huo kushindwa kuthaminiwa nchini, ikiwa
ni tofauti na nchi nyingine maarufu kupitia kikapu.
“Inatusikitisha
sana kwa kukosa nguvu ya kuendesha mashindano haya,kama unavyojuwa
tuanjiendesha kupitia mfuko wetu wa Shirikisho hapa hatuna mdhamini ,kwa kifupi
tuanjiendesha wenyewe tu, hii inaonyesha kiasi gani mchezo huu ulivyokosa thamani hapa nchini,”alisema.
Alisema
wanaitaka serikali kuwapa nguvu
na kuipa kipaumbele mchezo wa mpira wa kikapu kama wanavyosaidia michezo
mingine hapa nchini.
Mabingwa wa nne wa
michuano hiyo wataungana na mabingwa wa nne wa Zanzibar ambao wataenda kucheza
kwenye kombe la Muungano ili kupata mabingwa wawili watakao wataenda kushiriki
mashindano ya Afrika mashariki,kaskazini na kusini(ZONE 5).
No comments:
Post a Comment