Mahakama imeahirisha kesi inayowakabili raia 12 kutoka Iran.
Hatua hiyo imetokana na upande wa Jamhuri kudai kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Washtakiwa hao ni Kapteni Ayoub Mohamed, Buksh Mohamed, Fahiz Dauda, Khalid Ally, Abdul Somad, Saeed Sahury, Bashir Afraz, Morad Gwaram, Hazir Azad, Buksh Mohamed, Rahim Baksh na Abdul Bakashi.
Kesi hiyo iliahirishwa juzi na Hakimu Mkazi, Nyigulila Mwaseba.
Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Prosper Mwangamila, akisaidiwa na Wakili wa Serikali, Hamidu Mwanga, ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kutajwa.
Hakimu Mwaseba alisema kwa kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, kesi hiyo itatajwa Machi 13, mwaka huu na washtakiwa wataendelea kukaa mahabusu.
Awali, washtakiwa hao kupitia kwa wakalimani wa kutafsiri lugha ya Kiswahili kwenda Kipakistan na Kiiran, Maulana Mohamed na Zainabu Juma, walisomewa mashitaka yanayowakabili.
Mwangamila alidai kuwa kesi hiyo iko mahakamani hapo kwa ajili ya usikilizwaji wa awali na upelelezi ukikamilika itahamishiwa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Dar es Salaam.
“Mheshimiwa, kutokana na sababu hiyo, washtakiwa hawatakiwi kujibu chochote hadi kesi yao itakapokamilika upelelezi na kuhamishiwa Mahakama Kuu,” alida
>>NIPASHE
No comments:
Post a Comment