Wananchi 6,700 wa Kata ya Kilolambwani wilaya ya Lindi Vijijini, wanakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu wa chakula na kusababisha baadhi ya wananchi kula mizizi ya porini.
Kauli hiyo imetolewa na Diwani wa Kata hiyo, Salamu Matajabu pamoja na wenyeviti wa Serikali za Vijiji vya Nangole na Dimba wakati walipokuwa wakizungumza na timu ya waandishi wa habari kwa nyakati tofauti mjini Lindi.
![]() |
Ramani ya mkoa wa Lindi |
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Dimba, Abdalla Mbwana amesema hali ya chakula kwa wananchi wake ni mbaya jambo linaloweza kusababisha baadhi ya wakazi wa kijiji hicho kupoteza maisha kutokana na kukosa chakula.Naye Diwani wa kata ya Kilolambwani Salamu Mtajabu amesema kuwa tatizo la njaa katika eneo hilo limevikumba vijiji saba vinavyounda kata hiyo lililosababishwa na ukosefu wa mvua kwa misimu miwili mfululizo wa 2010/11 na 2012/13.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Dk.Nasoro Himidi amesema tatizo la upungufu wa chakula katika kata hiyo, ofisi yake inalitambua na tayari ameomba tani 19,000 za nafaka kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kitengo cha Maafa.
No comments:
Post a Comment