EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Wednesday, February 26, 2014

KESI TANO ZA RUSHWA KWA VIGOGO WA TANZANIA ZATAJWA NA TAKUKURU

Mkurugenzi Mtendaji wa Takukuru, Dk. Edward Hoseah.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru), imesema inatarajia kutangaza kesi kubwa tano za rushwa nchini.
Taasisi hiyo imesema kwa sasa inaendelea na uchunguzi na ukikamilika itatangaza kesi kubwa tano za rushwa nchini. Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Takukuru, Dk. Edward Hoseah, jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na NIPASHE jana.

CHANZO CHA TAARIFA HII AMBACHO NI NIPASHE lilitaka kujua ni lini Takukuru iitapeleka kesi kubwa mahakamani.
Akijibu swali hilo, Dk. Hoseah alisema uchunguzi bado unaendelea na ukikamilika itawaeleza wananchi kwa kuwa ni muhimu kujua wanahusika na kesi hizo.

“Bado tunaendelea kushirikiana na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kukamilisha zoezi hilo ambalo ni gumu. Katika mazingira yetu ya utendaji, ni lazima tukamilishe ndiyo tuzungumze na vyombo vya habari," alisema.

Alisema kuwa Takukuru itaendelea kupambana na rushwa kwani ndiyo jukumu lake na kuvitaka vyombo vya habari kushirikiana nayo katika kuwaelimisha wananchi juu ya madhara ya rushwa.  Dk. Hoseah alisema kwa sasa kumekithiri vitendo vya rushwa na watu wamechukulia kama ni sehemu ya maisha yao.

Aliwaomba wananchi waichukie rushwa kwa kuwa ndiyo suluhisho kwani kila mtu akiwa mla rushwa hatakuwapo wa kumkemea mwingine.

CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment