EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Tuesday, December 17, 2013

POLISI, WANANCHI WANUSURU KUZAGAA KWA MIL. 6 BANDIA .,,,,Na shafiimohamed Jeshi la Polisi Arusha



kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Leberatus sabasi


Jeshi la Polisi Mkoani hapa limemkamata mwanamke mmoja aitwaye Imelda Juma (20) Mkazi wa Sokoni One jiji hapa akiwa na noti bandia zenye thamani ya Tsh 6,140,000 (Milioni sita laki moja na elfu orobaini).

Akizungumza na SWACOTZ fisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas alisema kwamba tukio hilo lilitokea tarehe 13.12.2013 muda wa saa 10:00 Alasiri katika maeneo ya Kituo kikuu cha Mabasi mara baada ya jeshi hilo kupata taarifa toka kwa raia wema.

Kamanda Sabas alifafanua kwa kusema kwamba, siku ya tukio mtuhumiwa ambaye ni Imelda Juma alimtuma dereva wa pikipiki maarufu kama “boda boda” aitwaye Jamal Abdul ili aende maeneo ya Sakina Darajani kwenda kuchukua mzigo. Mara baada ya dereva huyo kufika katika eneo hilo aliukuta mzigo huo ukiwa pembeni ya pikipiki nyingine ambayo haikuwa na mtu.

Dereva huyo wa pikipiki aliuchukua mzigo huo na kuupeleka katika kituo cha mabasi cha Dar Express kama alivyoelekezwa na mtuhumiwa ambaye ndio mmiliki wa mzigo huo ili autume kwa mtu aliyefahamika kwa jina moja la Emmanuel ambaye inadaiwa yupo Dar es salaam. 


Wafanyakazi wa kampuni ya mabasi ya Dar Express waliokuwa ofisini hapo hawakuwa tayari kuupokea na kuusafirisha mzigo huo bila kuufungua ili wajiridhishe japokuwa dereva wa boda boda alikataa kufungua mzigo huo kwa madai kwamba mwenye mzigo alimwambia hasikubali mzigo huo ufunguliwe.

“Ndipo wafanyakakazi hao wakamshauri dereva huyo wa boda boda kama hataki ufunguliwe basi naye pia akate tiketi ili asafiri pamoja na mzigo wake mpaka Dar es salaam”. Alisema Kamanda Sabas.

Mara baada ya taarifa hiyo kufika katika kituo kikuu cha Polisi, askari waliweka mtego na kumkamata mtuhumiwa huyo Imelda Juma ambaye inasemekana alikuwa maeneo ya karibu na hapo.

Mpaka hivi sasa Jeshi hilo linaendelea kumhoji mtuhumiwa huyo ili kuweza kubaini mtambo unaotengeneza fedha hizo bandia huku pia likiendelea kumtafuta mtumiwa mwingine aitwaye Emmanuel.

Kufuatia tukio hilo Kamanda Sabas ameendelea kuwashukuru wananchi wa Mkoa huu kwa jinsi wanavyoshirikiana na jeshi hilo juu ya utoaji wa taarifa kwani fedha hizo kama zingesambaa mtaani kwa ajili ya matumizi zingedhoofisha uchumi wa nchi kwa kiasi fulani.

Aidha amewatahadhalisha wananchi wa Mkoa huu hasa wafanyabiashara kuwa makini na noti mbalimbali wanazozipokea toka kwa wateja wao, kwani wengine hutumia mwanya wa wingi wa noti kupenyeza fedha bandia.
$

No comments:

Post a Comment