EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Wednesday, February 26, 2014

VYAMA VYA USHIRIKA VYACHANGIA MILL 62 UJENZI WA SEKONDARI NACHINGWEA



MKUU WA MKOA WA LINDI KATIKATI..
Vyama vya ushirika vya kuuza na kununua mazao wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi, vimechangia zaidi ya sh.milioni 62 kwa ajili ya ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari ya wasichana wilayani humo.

Hayo yameelezwa na Afisa Ushirika wa wilaya ya Nachingwea Lameck Chota wakati alipokuwa akitoa taarifa ya ujenzi wa maabara hiyo, kwa mkuu wa mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila alipokuwa kwenye ziara siku tatu ya kukagua miradi ya maendeleo wilaya.

Chota amesema uongozi wa halmashauri hiyo kupitia idara ya ushirika iliviomba vya vya msingi kutenga shs 10 kwa kila kilo moja ya ufuta na korosho iliyouzwa katika vyama hivyo, ili kuchangia mradi wa ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari ya wasichana Nachingwea.
WANAFUNZI NA VIONGOZI MBALIMBALI WAKISHUHUDIA UJENZI WA JENGO LA SHULE (darasa)

Afisa Ushirika huyo amesema awamu ya kwanza ya msimu wa 2012/13 vyama vya ushirika nane kati ya 23, vilichangia ujumla ya shs milioni 42 ambazo zilisaidia kuanza mchakato wa kuanzisha ujenzi wa maabara hiyo.

Amesema ili ujenzi wa maabara hiyo uweze kukamilika zaidi ya shs milioni 39 zinahitaji, ambazo zinatarajiwa kuchangwa na vyama ambavyo havijachanga hadi sasa, na kuongeza kuwa wilaya hiyo ina vyama 23 na hadi sasa vyama 13 tu vimewasilisha michango yake.
                                        Chanzo, Mwanja Ibadi.LINDI

No comments:

Post a Comment