Na Mshamu Ngojwike,
Msanii Wa Zamani Wa Bendi Ya Vijana Jazz,Kida Waziri “Stone
Lady” Amesema Majungu,Wivu Na Ubinafsi Vilimfanya Ang’atuke Kwenye Kundi Hilo
Ambalo Lilikuwa Maarufu Miaka Ya 80.
Kida Ambaye Amerudi Tena Kwenye Mziki Wa Dansi Akiwa Kama
“Solo Artists” Huku Ataimba Nyimbo Za Zamani Ambazo Ameimba Wakati Yupo Vijana
Jazz.
Akizungumza Kwa Hisia Kali, Kwenye Jukwaa La Sanaa Ambalo Linafanyika
Kila Jumatatu Katika Ukumbi Wa Baraza La Sanaa Tanzania(Basata) Alisema
Pamoja Na Kupotea Kwa Muda Mrefu Vitu Ambavyo Vilimfanya Akae Pembeni Na Mziki
Kutokana Majungu,Wivu Na Ubinafsi Ambavyo Alikutana Nazo Kila Kukicha.
“Kipindi Kile Kwa Kweli Nilikuwa Kipindi Kigumu
Sana,Wanamziki Wenzangu Walikuwa Wananifanyia Visa Kila Kukicha Hadi Kupelekea
Niachane Kabisa Na Mziki Ambao Zaidi Ya Miaka 20 Nilkuwa Kando Na Tasnia Hii”
Alisema.
Waziri Alisema Awezi Kusahau Aliposhushwa Jukwaani, Na
Viongozi Wa Wajuu Wa Vijana Jazz,Ambapo Akikumbuka Upelekea Kumwaga Machozi.
Alisema Kwa Sasa Yupo Kwenye Maandalizi Ya Mwisho Ya Kuandaa
Albamu Ambayo Itahusisha Na Nyimbo Ambazo Aliziimba Zamani Akiwa Vijana
Jazz Akiwa Na Marehemu Baba Watoto Wake,Hemedi Maneti Ambazo Ameziongezea Ubora
Kama “Penzi Haligawanyiki” Sehemu Ya 1&2 Na “Mawifi Mnaninyanayasa” .
No comments:
Post a Comment